19 February 2006

Michuzi...Da Mija huyooo!


Kaka Michuzi, hapo katika picha nashangaa kusoma ujumbe wako kwamba wewe ni Meneja wa kikundi cha muziki wa asili cha Sisi Tambala, lakini mshangao wangu ulipunguka kidogo baada ya kukumbuka habari hii. Nilijiunga na kikundi hicho wakati kikianzishwa mwaka 1998, nikiwa mwanamke wa kwanza na pekee kundini, Enzi hizo tulikuwa watano tu lakini machachari sana ...wengine walikuwa ni Nanjuja Kibiriti, Salumu, Fadhili Mkenda na Kasembe Ungani. Duh! Michuzi umenikumbusha mbali.

Hapo kipindi cha nyuma nilishawahi kupandisha picha yangu, lakini naona imeshapotelea chini kutokana na kupandisha habari zingine, hapa ndipo umuhimu wa Wordpress unapokuja, Leo Michuzi usingepata taabu kuniomba picha, ungekong'oli tu kwenye maudhui ya picha ya Da Mija na kunikuta.

21 Comments:

At Sunday 19 February 2006 at 23:01:00 GMT, Blogger John Mwaipopo said...

Kakiunganishi ka 'alibamu' umekapeleka-ga wapi tujipigie-ge chabo wenyewe?

 
At Monday 20 February 2006 at 00:48:00 GMT, Blogger Jeff Msangi said...

Damija,
Ni faraja kusikia kwamba wewe ni mmoja wa waanzilishi wa Sisi Tambala.Nilikuwa nalipenda sana lile kundi na tafadhali kama bado lipo na unajua anuani yao tuwasiliane.Kuna uwezekano wa kuja hapa Toronto kufanya maonyesho wakati wa majira ya joto.

 
At Monday 20 February 2006 at 05:53:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Tafadhali. Kumbe Da Mija ndo wewe? (natania).
Sisi Tambala achana nao kabisa. Sisi Tambala wananikumbusha kundi la Wakenya wanaoishi Marekani la Jabali Afrika, nyimbo zao hasa zile za ngoma, filimbi, kayamba, n.k. bila magitaa na vinanda. Walipoanza kuingiza magitaa walinihuzunisha kiasi maana utamu wa nyimbo zao ulichujika. SIsi Tambala isije ikawa nao wameingilia magitaa, mavinanda?

 
At Monday 20 February 2006 at 05:57:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Ukitaka kuwaona Jabali Afrika, nenda hapa: http://www.jabali-afrika.com/

 
At Monday 20 February 2006 at 10:13:00 GMT, Blogger Mija Shija Sayi said...

Mwaipopo kile kiunganishi kilitoweka ghafla kutokana na matatizo ya kiufundi, nitakirudisha haraka iwezekanavyo.

Jeff sasa hivi sina namba yao nadhani wamebadilisha, lakini pia unaweza kuipata kwa Meneja wa kikundi bwana Michuzi.

Ndesajo asante kwa anuani ya Jabali la Afrika hapa nilipo nakula muziki wao.

 
At Monday 20 February 2006 at 12:12:00 GMT, Blogger mwandani said...

Sijui katika utamaduni wetu mwanaume akimsifu mwanamke asiye hawara yake - pasina nia ya kumtongoza - inakuwa vipi.

Saa nyingine natukanwa kwamba miye mshenzi, muhuni, sexist, bastard, hog na matusi mengine mengi, kwa kusifu urembo wa mtu.

Potelea mbali hata nikitukanwa. Picha yako Damija nimeipenda sana. Bila ya shaka we ni mrembo kweli kweli.

 
At Tuesday 21 February 2006 at 10:10:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Niliingilia masuala ya Sisi Tambala nikasahau hasa nilichotaka kusema.

Kumbe dunia yetu hii ya blogu ina warembo wa kukata na shoka. Chuma cha pua... Tuwakilishe mwanakwetu.

Mwandani: ni vigumu sana kwenye utamaduni wetu sifa kwa mwanamke ikaonekana kuwa ni sifa tu isiyo na nia ya pembeni. Kama vile urafiki kwa mwanamke kwa maana ya urafiki tu ni haba. Ukiwa na rafiki wa kike kwa maana ya urafiki tu washikaji zako watakuwa wanakucheka kuwa umezubaa.

Mija rudisha kile kiungo.

 
At Wednesday 22 February 2006 at 10:52:00 GMT, Blogger MICHUZI BLOG said...

damija nashukuru kwa picha. sina uhakika, lakini ingekuwa bora ungenitumia kwenye b.pepe, kuogopa hayo ya kina mwandani.... anyway, mradi wengi wamefurahia, akiwemo ndesanjo, nadhani ilikuwa kitu aali kuposti hiyo picha. hivi sasa sisi tambala tuna cd yenye nyimbo tatu, moja ikiwa 'katope' remix, 'afrika bara letu' na 'sisi tambala'. sio mbaya kwani 'katope' iliwahi kupanda chati na kuchuana na bongo fleva kwa wiki kadhaa katika nambari moja. afrika nayo twaifanyia promosheni ifikie huko. nitembelee baadae nitaweka picha yao ya karibuni. siku hizi kibiriti kabaki peke yake, na vijana saba ambao wanafanya kazi nzuri tu. vijana wengine waliondoka na kuunda afrikali na wengine zemkala. wote wanajitahidi kuendeleza mtindo 'ngwashala', ambao ni kama mtindo rasmi wa vikundi vya kiutamaduni, kama vile ndombolo, kwasakwasa etc. hivi sasa vikundi vinavyotamba ni pamoja na sisi tambala, simba theatre, oya theatre, afrikali, kyandu music, parapanda na zemkala. vingine vipo ila havina kasi sana. vile vile nakutaarifu kwamba kama ujuavyo bongo hakuna ukumbi mahususi wa sanaa. ila makumbusho ya taifa wameamua kujenga national theatre itakayokuwa na kila kitu. ujenzi utaanza punde kwani sida (sweden) wameshatoa pesa hivi sasa kandarasi zaandaliwa. utajengwa juu ya makumbusho ya taifa mtaa wa shaaban robert na hata jina hivi sasa ni national museum and house of culture.

 
At Wednesday 22 February 2006 at 21:28:00 GMT, Blogger John Mwaipopo said...

Tunashukuru Michuzi maana nawe sasa umekuwa mwanablogu (kabla hatujatafuta jina la Kiswazi). Utembelewapo nawe tembelea.

 
At Thursday 23 February 2006 at 07:34:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Michuzi: asante kwa taarifa zako za vikundi vya sanaa za maonyesho nchini. Ni vizuri kusikia kuwa mtindo wa ngwashala umekubalika.

 
At Thursday 23 February 2006 at 16:18:00 GMT, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

Da mija nimekukubali! uko bomba dada yangu! uliishaonana na makene hivi karibuni?

hongera kwa kufanya vitu vyako kati kati ya kiwanja! wengi huwa tunasema lakini kutenda ni ishu!!

mpaka usawa huu bado unatafuta wahabeshi?

 
At Thursday 23 February 2006 at 17:09:00 GMT, Blogger boniphace said...

Ndugu zangu nimekubali kuwa nina ndugu wanaoweza kunisemea yaani hata kiasi hiki, kuingia moyoni hapa nilipo na kufunua fikra zangu kisha kuzipaisha katika dirisha zitakiwapo fika. Mark huu utani huachi tu, lakini nakumbuka niliomba namba ya simu lakini nikaambiwa nitajibiwa baadaye kule kwa Michuzi nikabaki kusubiri! Cha kushangaza Michuzi kaomba picha ikawekwa haraka haraka na huyu Michuzi sijui ana kazi ngapi, maana uandishi, Picha, Blogu, kule Mbongo na katika sanaa alikuwa muigizaji na tena ana hisa, tufundishe Michuzi namna ya kuwa na wajasiliamali maana kwa namna hii unatisha sana.

 
At Friday 24 February 2006 at 13:07:00 GMT, Blogger MICHUZI BLOG said...

tena makene umenikumbusha. mie pia ni mwenyekiti wa sanaa klabu (cheki na kibiriti wa sisi tambala 0741 766676 ama james mbunju wa simba theatre 0744 570294 ama robino ntila 0745 319101 ama mgunga wa mnyenyelwa wa parapanda0744 6936623) klabu yenye vikundi 16 vya utamaduni. pia ni mjumbe wa kamati ya ushauri ya makumbusho ya taifa na nyumba ya utamaduni. makene, ukiangalia vyema si wengi wenye kupenda hayo mambo niyatendayo, angalau huku bongo, ndo maana ya kuhaha kote huko. lakini karibuni napumzika na kuchagua fani moja tu, uandishi wa vitabu vya tamthilia, vyenye nusu ukweli wa kazi hii ya uandishi. yote katika kuhangaika, kisha mambo ikiwa sawa naingia kwenye film production - stay tuned...

 
At Friday 24 February 2006 at 13:11:00 GMT, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

nafikiria itavyokuwa tamu....moja ya vikwazo ambavyo wengi wetu tuliotangulia hukumbana navyo ni kupata mwenzi mwenye fikra, mitazamo au uwezo hata wa ubongo tafauti na ulionao! ndio maana unakuta mtu kaacha kifaa ambacho wengi huona cha nguvu na kuhama upande! frequency haziingiliani!! THIS IS VERY SERIOUS!

kwa manaoanza safari hii ni kuchangamkia fursa hivyo msirudie makosa na kuishia kujilaumu ikiishakuwa historia!!!!

tunasubiri kadi nadhani hii ishu itawakutanisha wanablogu wote! - RAHA ILIYOJE! pia msisahau chelewa chelewa........... si wako!

cheers!

 
At Friday 24 February 2006 at 13:18:00 GMT, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

michuzi! utafika mungu akubariki! nakumbuka wakati haya mambo ya muziki wa kizazi kipya ulipoanza nilikuwa mmoja wa mapionner! nilifanya kazi na producer Marlon Linje! wakati huo waliokuwa wanajiita mapromoter kina Kim 'n the boys walikuwa wanakamua kweli vijana! tulifanya album lakini analysis ya soko ilitufanya tugwae na kuishia kushoot ITV na CTN! - ninachotaka kusema hapa ni kuwa unachofanya kina mchango mkubwa kwa nchi yetu kwani tunaporudi kuchukua nchi yetu wenyewe, haya mambo yote tutatengeneza na waliochukua kamba baada ya hapo watanufaika! nani alijua leo kina juma Nature watauza kiasi hiko? je kina mr II nao wangeacha leo hii si tungekuwa tunaliwa kununua kazi za wazungu katika utandawazi? na sisi hatuuzi zetu? - leo hii nenda klabu zote, madisco maband utanawazi umeliwa bongo upande huo!! natoa hoja: SEKTA NYINGINE TUIGE MBINU ZA WANAKIZAZI KIPYA KUPAMBANA NA UTANDAWIZI!

 
At Friday 24 February 2006 at 19:02:00 GMT, Blogger boniphace said...

Hapana Michuzi endelea na kazi zote maana inaonyesha namna thamani yako ilivyokubwa. Hakuna kuachia hao vijino pembe! Fanya kazi na suala la utamaduni hilo hapo una jambo mbalo halina siku litalipuka na kutoa faida kubwa kwa wengi. Nambie pia huo uwanja wa uandishi wa tamthiliya unaanza lini maana mimi kuandika nataka kuwen moja ya majukumu yangu hadi kufa. Smahani ninapozungumzia kufa hapa kuna watu wanahofu..ukizaliwa lazima kufa, huu ni wajibu na mimi nimeuweka kama moja ya mipango yangu ya dhati kabisa baada ya kuzaliwa.

Ok samahani Mija nashukuru kwa mail maana sikutarajia.

 
At Sunday 26 February 2006 at 14:58:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Mija toa namba hiyo. Acha unaa!

 
At Wednesday 1 March 2006 at 12:49:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Hongera kwa jitihada zako. Wakati mwingine huwa ni kazi ngumu kutafuta kujua historia ya watu mbalimbali, hasa wale mashughuli. Sasa kwa mpangu huu ulioanzisha wa kusakanya habari zao, na kuziweka katika blogu yako inaturahisishia sana kujua undani wao, hasa na siri za mafanikio yao. Lakini kitu kimoja ungetusaidia zaidi kutika kupata undani wao zaidi ya uliyoandika.( maana nafikiri si rahis kuandika kila kitu ulichopata kutoka katka tafiti zako mbalimbali ulizopitia kupata habari unazoandika)Tusaidie na kupata marejeo(reference)ya unakopata hizi habari. Ili iwe rahisi kwa anaetaka kusoma zaidi ya ulichotuandalia.

Natumaini umenipata

 
At Wednesday 1 March 2006 at 20:56:00 GMT, Blogger Mija Shija Sayi said...

Asante Jesica, nimekupata vyema. Umesema kitu cha msingi maana ni kweli huwezi kuandika kila kitu unachokipata wakati ukitafiti. Nitaanza kuweka na marejeo ya taarifa nitakazokuwa nikiziandika maana huwezi kujua katika marejeo hayo msomaji akakutana na kitu alichokuwa akikitafuta siku nyingi ambacho labda mimi sikukiona kama ni cha muhimu sana.

Nashukuru sasa Da'Jesica.

 
At Thursday 9 March 2006 at 14:12:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

hongera kwa kazi hii ya kutupa historia

 
At Sunday 15 April 2007 at 14:19:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Hi, I hope you read english. How are you? I found you via Google. I live in the Netherlands and I am looking for music from Sisi Tambala Band, especially a song named Katope. Could you help me with that?
Kind regards, Bram van der Velde
bram.bram[at]gmail[dot]com

 

Post a Comment

<< Home