Changamoto....Ni nani zaidi?.. Winnie au Graca?
Haya jamani, hivi karibuni nitawaleteeni harakati za maisha ya wanawake wa shoka Graca Machel na Winnie Mandela. Wanawake hawa wawili wana mambo mengi yanayoshabihiana katika harakati zao za maisha. Haya, kabla sijawaleteeni undani wao ninawapa changamoto hii ya kujaribu kumtafuta aliye zaidi ya mwenziye. Haya karibuni nami najiweka sawa.
18 Comments:
Swali gumu kidogo kwani watata uzuri wao au siasa zao. Lakini naweza jaribu kidogo. Kwa uzuri ungeweka picha za umri wao sawa sawa- yaani picha zao wakiwa vigori, twenties, 30s, 40s nk. Kwa picha ulizoweka umempendelea Madikizela.
Ndugu yangu Mwaipopo nimetafuta mno picha ya Graca akiwa kigoli, na katika zote angalau hiyo ndiyo anaonekana kigoli. Kuhusu shindano hili kwa kweli halina mipaka linagusa nyanja zote kuanzia siasa hadi urembo. Haya tuendelee.
Kwa urembo, kwangu mimi Winnie namba moja, lakini tuangalia msomo 'uzuri si hoja...' Mandela alimuacha kwa nini? tabia chafu. Huyu mwingine nampendea historia yake, sijua kama kuna mwingine aliyewahi kuolewa na Marais wawili wa nchi Tofauti kama yeye-Samora machel na Mandela. Hivi yawezekana, Mandela alianza naye kabla samora hajafa!
Winnie
Kuna tetesi kwamba kabla Machel hajamuoa alikuwa ni mchumba wa Edwardo Mondlane aliyekuwa kiongozi wa FRELIMO alivyofariki Machel akachukua. Halafu kuna habari zisizothibitishwa kwamba wakati Mandela akiwa Gerezani na Machel akiwa hai Machel alikuwa akitembea na Winnie. Lakini yote hayo ni maneno ya watu. Mandela pia bwana Regnald ana historia nzuri ya kuacha wanawake. Huyu aliye naye ni wa tatu
Graca! analipa sana! ukitaka picha yake tafuta kile kitabu cha picha alikitoa nadhani sir George Kahama sijui kilikwa kina picha za Nyerere au Msiba wa Sokoine! kuna picha moja Graca alikuwa amepozi na mchonga nadhani.....japo nilikuwa bwa mdogo nilimzimia pale pale!
natamani kuona picha yako, da'mija, ukizingatia mi ndiye meneja wa sisi tambala, nadhaniwajuanasemanini...
Da Mija, unaweza kumwambia Graca apunguze ukubwa wa mawani yake? Nadhani mawani yale huwa yanampunguzia maksi. Au?
Ngoja nifikirie nani zaidi...hivi ni kiitikadi, kikazi, kisura, au vyote?
Michuzi tazama kapicha ka Da'Mija kunako albamu yake hapo kwenye viunganishi. Yuko 'Bomba Mbaya' babake!
Naona keshakitoa kiugnanishi cha 'alibamu' yake
Miye wangu Winnie! Maelezo zaidi baadaye.
F MtiMkubwa Tungaraza.
Kwa staili ya picha hizi mimi sisemi maana domo lilianza kubaki kimya, nikatazama chini na kuchimba sakafu. Nikatupa tena jicho katika skirini ya kompyuta yangu na mwisho nikakuza picha hiyo full skrini. Bado sikuridhika nikaona niiweke kwenbye CD ili nikaprinti kabisa na kuitunza. Lakini baadaye nikagundua nilikuwa naota tu...kweli Mija sina hali wala mali. Kwendako Hisani hakurudi Nuksani, nipe siku nitasemea Kasrini kwangu.
Inda nataka uthibitishe kuwa mimi ninaacha wanawake na niliye naye ni tatu
Swali zuri Reginald.
Kama nimemuelewa vizuri bwana Idya, si kwamba anasema bwana Miruko ana mke wa tatu sasa, ila anamueleza bwana Miruko kwamba, kwa Mandela huyu ni mke wa tatu na si wapili kama wengi wanavyojua.
Sijui kama niko sawa, kama siko sawa basi Idya inabidi uthibitishe tamko lako.....
Da Mija upo sahihi kabisa namweleza Mandela na si Miruko.
wajameni! kwa taarifa yenu! yule bwa mdogo alikuwa anamsaidia mandela wakati amefungwa na kujichana michuzi ya ANC na maza hivyo kupelekea kuvunjika kwa ndoa ya winnie na mandela anaitwa Dali Mpofu na sasa ni CEO wa South African Broadcast Coorporation! SABC. wakati huo kijamaa kilikuwa kikoo varsity! - inawezekana kabisa msaada huu alioutoa ndio umempa kapost!haya mambo bwana!
mnaniruhusu kuwahamishia kwangu ili niweke picha latest ya mandela akiwa na wote wawili hivi karibuni? we mwaipopo usipotoshe umma. utajaji vipi kwa picha za zamani. halafu ndesanjo usivunge. jibu unalo. ugonjwa wako kwa kinamama naujua, ingawa ntakuachia useme mwenyewe kabla sijakuumbua.
Post a Comment
<< Home