26 December 2005

Kibanda cha majadiliano ya neno blogu kwa kiswahili.

Wasomaji na wanablogu wote, ili kufanikisha zoezi la upatikanaji wa neno blogu kwa kiswahili, nimeona niweke kiungo ambacho sisi wote tutakuwa tunakutanikia, Kaka Ndesanjo alitoa wazo hili na Kaka Mwandani akatoa kiungo hiki kwa Kaka Jeff, Da Mija akakibandika. Kiungo hiki ambacho kina kichwa cha habari "BUNGABONGO YA NENO BLOGU KWA KISWAHILI" nimekiweka upande wa kulia juu ya Kichwa cha habari "Blogu Motomoto". Ingekuwa ni vyema basi yale yote tuliyoyapendekeza tuyahamishie huko kibandani.

1 Comments:

At Tuesday, 27 December 2005 at 00:47:00 GMT, Blogger Ndesanjo Macha said...

Shukrani zote zikujie kwa kuweka kiungo hicho. Tutafuata mfano huo na kuweka kwetu. Sasa kuhusu utaratibu wenyewe: tutaweka tarehe ya mwisho? Tutapiga kura?

 

Post a Comment

<< Home