01 January 2006

Bibi Anna Claudia Senkoro atufungulia mwaka.


Jina Anna Senkoro si geni tena masikioni mwa Mtanzania yeyote yule, mama huyu ndiye mwanamke pekee aliyeamua binafsi kuthubutu kugombea nafasi ya kuliongoza taifa zima la Tanzania katika awamu ya nne. Kutokana na uthubutu wake nimemchagua kutufungulia mwaka si kwa sababu nyingine yoyote ile bali ni kwa UTHUBUTU aliouonyesha. Binafsi ninaamini katika kujaribu na siamini katika kuogopa au kusikilizia. Sijui wenzangu mnasemaje juu ya uchaguzi nilioufanya? kama kuna lalamiko lolote naomba lisisite kunifikia. Kwa asiyemjua kwa sura ndiye huyo hapo juu.

2 Comments:

At Monday, 2 January 2006 at 10:35:00 GMT, Blogger mark msaki said...

binafsi ninampongeza sana huyo mama kwa alichofanya. ukiacha mbali kina tibaijuka waliojaribu ccm wakapigwa kushoto siku zilweeeeeeeee. hii ina maana kuwa upinzani unalea demokrasia

cheers

 
At Tuesday, 3 January 2006 at 02:09:00 GMT, Blogger John Mwaipopo said...

Yaani hapo DaMija umepatia kabisa. hata ingekuwa kufunga mwaka jana. Tena ingependeza sana kwani uchaguzi ndio ulifanyika. Hakika ningalikuwa Bongo mimi ningalimpigia kura yangu huyu mwanamke, si kwa sababu yoyote ile bali kwa kuonyesha kuwa na wanawake nao wanaweza.

 

Post a Comment

<< Home