08 December 2005

..".WABARIKI VIONGOZI WAKE"...MtiMkubwa umetoa tena dukuduku lake!

MtiMkubwa kama kawaida yake umetoa tena dukuduku lake hili hapa chini.

"Miye naupenda sana wimbo wa Taifa wa Tanzania (Mungu Ibariki Afrika). Wimbo huu siye Watanzania tumeukopa toka Afrika ya Kusini. Nyimbo hii ni nzee sana ilitungwa kunako mwaka 1897 kwa hiyo una miaka takribani mia moja na kumi na moja! (111)! Muziki wa nyimbo hii ni utunzi wa Hayati Enoch Sentonga, ambapo maneno yake yaliyotungwa na Hayati Enoch Sentonga na baadaye yakaja kukarabatiwa na Mshairi Samuel Mghayi. Wimbo hatujaukopa Watanzania tu, na Wazambia nao na Wazimbabwe hali kadhalika. Lakini sijui ni kwa sababu gani Wazimbabwe waliuacha wimbo huu na kuchukua mwingine.

Wimbo huu huwa unanipa na kunitoa raha pale unapofika kwenye mstari wa "WABARIKI VIONGOZI WAKE"! Ukifika hapo huwa unanikumbusha sura za viongozi walionuna wakiwa wamesimama pale mein stend, neshno stedium, Huku askari wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na chipukizi wa chama wakiwa wamekauka juani na saluti kali. Halafu na Watanzania wapenda amani na utulivu, Wafanyakazi, Wakulima na "Wazururaji" wakiwa wametanda kwenye sehemu zingine za uwanja wakishiriki kwenye hiyo ghafla aidha kwa ridhaa zao au vinginevyo. Miujiza ya Tanzania Mei Dei au SabaSaba wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na hai-skuli wote wanashiriki kikamilifu.

Turudi kwenye Mungu Ibariki Afrika, hususani pale kwenye mstari wa "WABARIKI VIONGOZI WAKE". Hapo nadhani ndipo Watanzania tulipopewa uwezo wa pekee wa kuweza kumtia kizunguzungu Mwenyezi MUNGU! Maanake Mwenyezi Mungu akiwatazama hao viongozi tunaomuomba awabariki, Mwenyezi Mungu mwenyewe anapata kizunguzungu. Lakini dua letu sio kama linaishia kwa viongozi wetu wa Tanzania peke yake, bali tunawaombea na majirani zetu kama Waganda wakati ule wakiwa na Idd Amini Dada, Malawi na Dr Hasting Kamuzu Banda, Zaire na Mobutu Sese Seko Kuku Mbwendu wa Zabanga, Viongozi wazalendo wa Wahutu na Watutsi wa Rwanda na Burundi, kina Alphonso Dhlakama kiongozi wa chama cha RENAMO cha Msumbiji. Dua zetu pia zilikuwa zinawaombea kina Eyadema, Omar Bongo,Paschal Lisouba, Jean Babtist Bokassa, Macias Nguema, Mfalme Hassan, Jaffar Nimeir, Omar Bashir na Hassan Tourabi, John Voster, Tommy Ndabaningi Sintole, Abel Muzorewa, Morgan Tsivangirai, Jonas Savimbi, Gatsha Mongasuthu Buthelezi na wengineo wote wamo kwenye dua hiyo ya "WABARIKI VIONGOZI WAKE".

Leo 09 disemba Watanzania tutaimba tena MUNGU IBARIKI AFRIKA, WABARIKI VIONGOZI WAKE,...Wakati tukiimba hivyo tutazame jirani yetu Kenya. Tumuombe Mwenyezi Mungu AWABARIKI VIONGOZI WAKE. (Kuna neno nimetaka kulisema lakini nimelimezea) kama hapo chini.
BONYEZA HAPA upaone hapo chini.

4 Comments:

At Friday 9 December 2005 at 10:30:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Katika historia ulikuwa ukipata ngapi?

 
At Friday 9 December 2005 at 15:47:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Kwa ninavyojua neno'kopa'lina maana ya kuchukua kitu kwa mtu kwa makubaliano ya kukirudisha. Tanzania imekopa wimbo na imesahau kuurudisha, Wasauzi kwa hasira ya kutokulipwa deni lao wameivamia nchi.

 
At Saturday 10 December 2005 at 21:33:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Da'Mija hapa umepatia sana. Nilikua nafahamu Enoch Sentonga kuwa ndiye mtunzi wa kawimbo ketu ka nchi, ingawaje makaburu yakamkatili maisha babadaye. Ila sikuwa najua nani alikarabati katika Kiswahili. Yaani asante sana kwa kuchimbua na kuweka hadharani. Hoja yako inashikika lakini katika safu ya viongozi uliowamensheni (kwa kejeli ya kuwa madikteta (mawazo yangu)wamo wakombozi halisi).Kazi njema.

 
At Tuesday 20 December 2005 at 11:22:00 GMT, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

hatukati tena hizi drama! tunachotaka ni uhuru kamili na demokrasia ya kuamua mambo yetu wenyewe! haya mambo ya kusimamishwa juani! kwamba chama changu ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yakio!!!!!akuuuuu!!!

 

Post a Comment

<< Home