01 November 2005

Ugumu wa mwezi mtukufu.

Majuzi nilipata habari hii ya ugumu wa Ramadhani kutoka katika vyanzo vyangu vya habari vilivyoko matawi ya kati. Kwamba kuna huyu mlevi ambaye naye katika mwezi huu hakuwa na namna ya kuukwepa ila kuungana na waumini wengine katika kufunga na kutokugusa pombe kwa mwezi mzima. Jioni moja mlevi huyu alikuwa msikitini akisali, sala yake ilikuwa kama ifuatavyo;

"Ewe Mungu, ifanye Ramadhani kama world cup, ije mara moja katika miaka minne na kila mwaka ije katika nchi nyingine! Amina.

Kwa mtazamo wangu baada ya kuipambanua sala hii ndani nje niligundua kwamba watu wengi sasa hivi hawajui ni kwa nini wanafunga na wanafunga kama sheria na ndio maana huweza hata kuthubutu kuomba ije mara chache, lakini kama wangekuwa wanajua kule kufunga ni kwa manufaa yao wenyewe basi wangeomba hata iongezwe. Hapa nadhani msasa wa haja unahitajika maana kujisahau nako kupo duniani.

1 Comments:

At Wednesday 2 November 2005 at 09:20:00 GMT, Blogger Indya Nkya said...

Da Mija acha vituko. Usitake kutuvunja mbavu wengine. World Cup na mfungo? Hiyo kali. Kama unavyosema ni kweli kufunga hata kama huamini kidini ni utaratibu mzuri sana wa kurekebisha afya yako.

 

Post a Comment

<< Home