07 December 2005

Jamani ninaomba ruksa yenu!

Ndugu wasomaji, Kuna hili suala nyeti sana katika ulimwengu huu, suala la MAHUSIANO YA KIMAPENZI. Suala hili ingawa ni nyeti sana na linalomhusu karibu kila mtu mzima hapa ulimwenguni, lakini ni suala la mwisho kabisa katika kuzungumziwa kwa UWAZI, imekuwa ikioneka kama ni ukosefu wa adabu kulijadili hadharani, Matokeo yake watu tumekuwa tukilivamia tu bila kuchukua tahadhari zozote au bila kujua tunacho kihitaji hasa katika mahusiano hayo na hivyo kusababisha wengi wetu kuishia matatizoni.

Binafsi nimekaa nikaona si vyema kuendelea kulifungia macho suala hili, kuna haja ya kuanza kulizungumza kwa uwazi huku wote kwa pamoja tukishirikiana katika kubadilishana mawazo. Nia hasa ikiwa ni kufunguana akili ili tuweze kuwa makini zaidi wakati tunapoamua kuingia katika mahusiano hayo.

Hivyo basi sina budi kuomba ruksa yenu ili kwa pamoja tukubaliane kuliweka sebuleni jambo ambalo ambalo linaonekana ni la chumbani.

Kuna mambo mengi ya kuyajadili, lakini labda tuanze na hili dogo.

NI VITU GANI MWANAUME HUTEGEMEA KUVIPATA KUTOKA KWA MWANAMKE? NA MWANAMKE KUTOKA KWA MWANAUME?

Wasomaji, ninaamini mjadala huu utatusaidia katika kujitambua zaidi, na kuwa makini wakati tunapotaka kufanya maamuzi.

5 Comments:

At Wednesday, 7 December 2005 at 10:01:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

nasema ruksa!

 
At Thursday, 8 December 2005 at 03:28:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Wanawake wanataka faraja na mahusiano na wanaume wanataka raha na uroda haraka haraka. Sitanii.

 
At Thursday, 8 December 2005 at 07:00:00 GMT, Blogger Mija Shija Sayi said...

Nakubaliana nawe kwamba wanaume hupeta uroda tu tena haraka haraka tofauti na wanawake. Lakini huoni kwamba hili linasababishwa na kutokuwa na utaratibu wa kuwafunda wanaume kama ilivyo kwa wanawake?..halafu unaonaje kama wanaume nao wangekuwa na kitchen party yao kabla ya kufunga ndoa ili wapate mafunzo juu ya kuishi na mke? nina hakika wanaume wengi hawajui kwamba kuishi na mwanamke kunahitaji ufundi na kama usipokuwa nao basi jiandae kusaidiwa na na wenye nao. Sasa ili kuepukana na hili labda mafunzo kabla ya ndoa kwa wanaume yangeanzishwa.

 
At Thursday, 8 December 2005 at 07:49:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

wanaume wanafundana mpirani au kijiweni tangu wakiwa na miaka 12.
Na kila mwanaume hakosi kujisifu umahiri wa mapenzi akiwa kilingeni. Lakini mambo mengine hatuyawezi tu, tunayaona kwenye sinema za kihindi na tunaanza kuyasikia tukijitumbukiza kwenye mahusiano ya muda mrefu.
Suala la uroda kwa wanaume na suala la wanawake kuchukua muda mrefu hayo ni maumbile.
mie naona wanawake wangeji-adjust kidogo kuwaridhisha akina baba kwa shamra-shamra mbali mbali(sijui unanielewa?)
halafu utaona faraja na mahusiano yatakayofuata

 
At Friday, 3 October 2008 at 18:59:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Kwa ufupi..... mwanaume anategemea viuno kutoka kwa mwanamke. Na mwanamke anategemea michomo kutoka kwa mwanaume.

 

Post a Comment

<< Home