27 October 2005

Mchina amtwanga ''hedi'' mbantu na kuzirai.

Jamanieee! sasa watanzania tumezidi, inakuwaje mgeni anayekujia nyumbani akutawale wewe mwenye nyumba??!! na wewe mwenye nyumba unakubali tu ni wogaaa au utumwa?

"MtiMkubwa" Fidelis Tungaraza, amenipatia habari hii niilete kwenu wasomaji ili kwa pamoja tuweze kujadili tatizo letu ni nini hasa, ameanza kwa kuhoji hivi
Mimi nilifikiri kizazi cha wale watanganyika waliombeba Dr Livingstone tena akiwa kafa kilikwisha! La hasha! Kumbe wajukuu zao bado tupo na tunaendeleza waliyoyafanya! Nilipokuwa chuo cha sanaa Bagamoyo, nilikuwa nikienda kanisani na kutazama pale mahala aliposimama wale watanganyika waliombeba mfu Dr Livingstone na kuwaambia wazungu wenziye kwamba "..Bwana amefariki.." Nilikuwa sipati majibu kwamba: Wale watanganyika walikuwa na utu sana??, Au walifanya vile kwa sababu walikuwa wanataka walipwe mishahara, marupurupu, mafao na pensioni zao kwa kukileta kidhibiti cha maiti?? Au walimpenda sana hayati Dr Livingstone? Au walikuwa wafanya kazi watiifu na waaminifu kwa mwajiri wao? Au walikuwa kama waswahili wasemavyo mafala?? Au walikuwa wapumbavu kupindukia?? Au kama uchawi upo walikuwa wamelogwa??

Siku zilizopita nilikarahishwa na habari kama hii kwenye gazeti la Dar Leo, (www.bsctimes.com). Habari hiyo ilikuwa na kichwa cha habari "ASKARI WA KIINGEREZA WAUA CHANGUDOA". Habari hiyo niliituma kwa baadhi yetu na na kwa Mheshimiwa Waziri Omar Mapurina Balozi Abdulkadir Shareef ili kwamba ichukuliwe hatua. Sijui kama kuna hatua iliyochukuliwa. Leo nimekumbana tena na habari za kabila hiyo hiyo yenye kichwa cha habari. MCHINA AMTWANGA AMTWANGA 'HEDI' MBANTU NA KUZIRAI. Kuna tusi limeniijia lakini nalihifadhi, hivi ingekuwa MBANTU KAMPIGA 'HEDI' MCHINA NA KUZIRAI ndani ya mitaa ya Beijing huyo Mbantu angekuwa hai mpaka saa hizi?? Leo imenipasa kusema kwamba wajukuu wa wale Watanganyika bado tupo, baada ya kukumbana na taarifa hii kwenye gazeti la Nipashe. Hebu jisomee mwenyewe hapa.

2 Comments:

At Thursday, 27 October 2005 at 16:36:00 BST, Blogger mwandani said...

Ni afrika tu ambapo mwafrika anaweza kupigwa na mgeni na mgeni akaachiwa aende zake...

 
At Friday, 28 October 2005 at 09:07:00 BST, Blogger Indya Nkya said...

Unajua kuna matatizo mengi sana. Sheria za kazi zilizopitishwa na bunge mwaka jana zinapendelea wawekezaji ambayo kwa definition ya Tanzania ni lazima atoke nje. Kuna wakati nasikia kaburu mmoja aliwaambia wafanyakazi wa Tanzania kwamba Zamani mlikuwa mkiimba Kaburu matata hiyo..Sasa mtakoma. Halafu hakuna anayeonekana kujali. Au jamani sisi ni wavivu na wabishi kiasi kwamba Mchina hawezi kuvumilia huo uvivu. Lakini hata kama ni hivyo, unamtwanga mtu kichwa?

 

Post a Comment

<< Home