28 October 2005

Uchaguzi wahailishwa....

Kutokana na kifo cha mgombea mwenza wa chama cha CHADEMA, Bwana Jumbe Rajab Jumbe uchaguzi wa Tanzania umehailishwa kutoka 30 oktoba hadi 18 disemba. Soma hapa na hapa upate habari zaidi. Poleni CHADEMA, poleni wananchi. Kifooo kifooo kifo hakina huruma!!

5 Comments:

At Friday, 28 October 2005 at 11:36:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Kufa kufaana! Kuahirishwa kwa uchaguzi kutawaafa sana wale waliokoseakosea kwenye kampeni kurekebisha makosa. Kutawafaa sana wapambe wa wagombea kwa sababu kama nyumba ilishafika tofali la mwisho sasa watapaua. Kutawafaa walala hoi kwa sababu mapilau, mitori, pepsi, mbege, kimpumu, kindi, komoni za kampeni vitaendelea kumiminika kwa wiki zingine tatu: walala hoi wanapiga dua afe mgombea mwingine baada ya tarehe 18.Novemba. Neema zizidi kuwamiminikia.

Kina Kikwete, mwenzake Mbowe, Profesa Lipumba, Maalim Seif, Mchungaji Mtikila, Bi Senkoro, Profesa Mvungi, Profesa Shayo nawaonea huruma na kuwaombea wazidi kuwa na nguvu na stamina kwa sababu ngoma imezinduka upya na lazima waendelee kucheza katika kasi ile ile wakilegeza kidogo athali zake wanazijua.

Wagombea wengine nao hii ni fursa adimu ya kutafuta helikopta. Mpango wa kusafiria usafiri usio wako ulimpandisha Mheshimiwa Sumaye kwenye kiberenge. Mambo ya uchaguzi jamani!!! Hebu pigeni picha Mheshimiwa Sumaye na Kaunda suti yake au shati lake la kijani la CCM kachutama kwenye Kiberenge!

 
At Friday, 28 October 2005 at 14:08:00 BST, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Hii ni kama ahueni kwa watu wengine sisi tunaendelea kula manywaji.Mapaka dec 18?

 
At Friday, 28 October 2005 at 15:25:00 BST, Blogger boniphace said...

Gharama hizi za uchaguzi atazibeba nani! fikiri hapo na jibu lake rahisi sana, subiri serikali ijayo na utaona athari ya hili. Kama mgombea alilazwa karibu muda wote wa Kampeni kwa nini busara isitumike, tutaishi kwa kuabudu maandishi tuliyoandikiwa hadi lini! Wanafunzi vyuo vikuu hawanma fedha za mikopo, hospitali hakuna madawa, wafanyakazi hawana malipo safi sasa huyo mzee aliyetelekezwa Hindu Mandal na chama chake analeta hasara kwa nchi ya bilions of money? Kazi imeanza ya kufuta katiba na kuandika mpya

 
At Friday, 28 October 2005 at 15:56:00 BST, Blogger Indya Nkya said...

Safi sana Makene. Pesa zenyewe ndizo hizo za kutembeza bakuli. Nasikia jana walikaa masaa manane wakiongea na hao wanaoitwa wahisani kuangalia kama wanaweza kufadhili. Hizi Katiba za kufuta jina la nchi iliyoendelea na kuweka la kwako ndio ujinga wake. Kwa nini katiba isizingatie mfuko wako bwana? maandishi yamewekwa na binadamu na hutenguliwa na binadamu.

 
At Friday, 28 October 2005 at 18:06:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Naam,

Sasa tunaanza kuafiki hoja ya Mchungaji Mtikila kwamba wagombea wapimwe afya zao! Alipotoa hoja hiyo kwa fikira za haraka haraka ikaoneka kama anambeza mgombea mmoja binafsi.

Samahani lakini kwetu sisi si vitabu wala busara inayotumika bali ni 'utaratibu'. Ingelikuwa kama tunafuata vitabu na busara ingekuwa inatumika tusingelikuwa jinsi tulivyo.

Tukilifuatilia suala la pesa na gharama za kuahirishwa uchaguzi tutakuta kwamba hata ukiaihirishwa mara nyingine zitakuwepo pesa za kugharamia uchaguzi. Kwa kawaida huwa hatuna pesa za mishahara ya walimu lakini huwa na tuna pesa za mishahara ya wabunge. Hatuna pesa za kununulia tolitoli(ambulance) za hospitali, matrekta ya wakulima, au magari ya polisi lakini tuna pesa za kununulia mapajero ya wakuu wa mikoa wabunge, mawaziri, na ndege ya Rais. Hatuna pesa za kupanulia ujenzi wa nyumba za wananchi, majengo ya sekta za afya na elimu lakini tuna pesa za kujengea majengo ya bunge jipya na makao makuu mapya ambako hakai kiongozi wala haamii Mtanzania yoyote. Ndugu zangu hii ni mifano michache kati maelfu na haya yote hayatokani na kufuata vitabu au busara bali ni kutokana na kufuata 'utaratibu'.

Aliyetoa hoja ya kufa kufaana katoa hoja nzuri. Wengi wa hao wabunge wakati pekee wa kufaidi nao ni pale wanapokuja kuomba kura. Wakishazipata na kuanza kujipitishia posho, mishahara, marupupu, na pensheni za kutisha (maVX au maPajero?, shilingi milioni 20 au 40 za kumaliza kipindi cha miaka mitano? Achilia mbali posho za vikao ambavyo hawana lolote la kimsingi wanalochangia au kuamua)Hawakuletei kula wala maji sahau kukuletea madawa kwenye dispensari au kliniki za vijijini au kujenga darasa au kuleta madawati na vitabu kwenye shule za vijijini. Nimejisikia kutaja majina ya wabunge fulani ili kuipa nguvu hoja yangu lakini kama ukipenda naomba tuwasiliane tujadili. Hao wabunge fulani wamo bungeni tangu enzi ya baraza la kutunga sheria, na wengine waliodandia ubunge toka miaka ya sitini, sabini, na themanini lakini jiulize kama wanayajua maisha ya watu wa majimbo yao ya uchaguzi achilia mbali maisha ya Mtanzania wa kawaida.Hata mimi akinitokea mbunge wa kabila hiyo simuachii nampiga kisukumizo ili na mimi nikifaidi kile alichochota toka kwenye mchango wa Watanzania wengine wote.

Jamani kwa herini, miye basi.

F MtiMkubwa Tungaraza.

 

Post a Comment

<< Home