03 October 2005

Binafsi sikubaliani kabisa na adhabu hii....

Siwatetei na wala sijapendezwa na kitendo walichokifanya wanafunzi hawa mabinti wawili. Lakini tukiangalia kwa jicho la undani adhabu hii ya kufukuzwa shule kwa wanafunzi hawa tena wakiwa wamebakiza juma moja la kufanya mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne, imetolewa bila kuangalia madhara yake kwa watoto hawa hapo baadaye. Kwanza kabisa tumesha poteza labda maprofesa wa kesho, maana huwezi kujua mikakati yao ya maisha walikuwa wameipangaje, pili kitaifa badala ya kubembeleza watoto wasome ili tupate taifa lenye watu waliofunguka fikra, sisi tunawakatiza kwa makosa yanayotokana na utoto wao (nina hakika wako chini ya miaka 20, na hiki ni kipindi kibaya kwa vijana kutaka kujaribu mapenzi hapa na pale) wenzetu wa nchi zingine hawaleti mchezo katika masuala ya elimu, hivi vimakosa vya mpito hutatuliwa kwa njia nyinginezo ambazo pia humjenga mtoto. Tatu huko jamiini wanakokwenda ndio watakuta wameshanyanyapaliwa tayari, ile kufika tu na vidole kila mtu juu yao, hapo tumeshaua tayari kujiamini na kujidhamini, na kutokana na umri wao wataanza kujiona kwamba hawafai na si kitu katika jamii na hapo huwa ni ngoma kumsawazisha mtu.

Sawa, lakini na hao wanaume, watu wazima na wake za watu wamepewa adhabu gani?
Kisa chenyewe hiki hapa.

4 Comments:

At Monday, 3 October 2005 at 21:17:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Interesting blog you have here, I landed here on accident. I was searcing for something else and came across your site. I found it pretty interesting and entertaining. I got you book marked.

I will pop back in from time to time to see what you have new here.

My site is a bit different than yours, but just as entertaining and educational, I run a penile extenders related site pertaining to penile extenders related articles.

 
At Tuesday, 4 October 2005 at 08:31:00 BST, Blogger Indya Nkya said...

Japo hujatueleza kwa undani chanzo cha habari hiyo (badhani ume "assume" kwamba kila mtu kaisoma),kufukuza mtoto shule si suluhisho kabisa. Isitoshe sasa hivi tunawaacha watoto wetu kuogelea hovyo katika dunia hii yenye kubadilika haraka. Wazazi wanawaachia waalimu kazi ya malezi na walimu wanadhani ni kazi ya wazazi. Kwa kutumia lugha ya kikoloni nitasema: "there is no complementarity between parents and teachers in the process of bringing up our kids". Wakati mwingine tunadhani dini zitawasaidia kuwa na maadili. Tukishaona wanaenda kwenye nyumba za ibada, tunakaa na kustarehe kwamba watoto wanapata maadili. Ni lazima kuziba pengo la malezi ya watoto. Malezi lazima yabadilike kutokana na dunia inavyobadilika kwa kasi.

 
At Tuesday, 4 October 2005 at 08:34:00 BST, Blogger Indya Nkya said...

Samahani sana. Nilishikwa na jazba kabla sijamaliza kusoma. Chanzo cha habari nimekiona.

 
At Monday, 17 October 2005 at 05:49:00 BST, Blogger Ndesanjo Macha said...

Jambo hili kidogo kama lile la kufukuza watoto shule wakipata mimba. Yaani tunaona ni vizuri kuwa na taifa la wazazi (watakuwa wazazi wakishajifungua) wasio na elimu. Watoto hao tumboni wana kosa gani hadi tuwape adhabu ya kuzaliwa na mama wasio na elimu?

 

Post a Comment

<< Home