09 April 2006

Unamfahamu mwanamke wa kwanza kuingia katika baraza la mawaziri la tanzania?


Pengine kuna haja ya kuwajua mashujaa wetu wa kwanza kabisa waliojitolea kwa mioyo yao yote kuipigania nchi yetu. Wako wengi ingawa leo hii wanasikika wachache tu. Swali langu au tuite mtego wangu wa leo ni kumtaja mwanamke wa kwanza kuingia katika baraza la mawaziri Tanzania wakati huo ikiwa ni Tanganyika na je ni ipi nafasi yake leo katika Tanzania yetu, je anaenziwa kama kina Karume na Nyerere hadi kupewa siku za mapumziko? Kumbuka enzi hizo hadi uweze kushika nafasi ya uwaziri ni lazima harakati zako za kupigania uhuru zilikuwa na za kiwango cha juu.

JE MWANAMKE HUYU NI NANI?

10 Comments:

At Monday 10 April 2006 at 08:39:00 BST, Blogger mzee wa mshitu said...

Mija ngoja nijaribu kutegua mtego huu, nadhani kuwa ni Tabitha Siwale kama sikosei ndiyo maana nasema nadhani. Kama nimekosea wenzangu watajaribu na kama ni yeye basi haifai kabisa kuwaenzi waasisi kwa staili ile!

 
At Monday 10 April 2006 at 13:47:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Ndugu Charahani,

Sina hakika kama umepata. Kwa sababu alipoingia Mama Thabita Siwale (Ardhi, Nyumba, na Maendeleo Mijini) 1975 aliingia na Julie Manning (Sheria) kwa hiyo palikuwepo wanawake wawili kwa mpigo!

Kama nina kumbukumbu nzuri Bibi Titi Mohamed alipata kuwa Waziri Mdogo wa Afya kuanzia mwaka 1962. Pia Bibi Lucy Lameck aliwahi kuwa Waziri Mdogo wa Ushirika na Maendeleo ya Jamii kati ya mwaka 1965 hadi 1970.

Kumbukumbu zangu katika hili zinaishia hapa. Mija, tukishindwa wote tutakupa mji!

F MtiMkubwa Tungaraza

 
At Monday 10 April 2006 at 20:26:00 BST, Blogger John Mwaipopo said...

Tungaraza bongo inafanya kazi.

 
At Tuesday 11 April 2006 at 17:29:00 BST, Blogger MICHUZI BLOG said...

naomba nisitie neno. da mija, ukitaja mshindi na jina la huyo mama nitakuzawadia picha yake uiweke. ila nami nakumbusha kwamba kuna mtu anaitwa joyce mhaville yeye ni kibosile wa itv na redio wani. nadhani ni mwanamke wa kwanza kushika nyadhifa ya juu kwenye chombo chochote cha habari, tena kwa muda mrefu

 
At Wednesday 12 April 2006 at 13:07:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Mghh, Michuzi hebu cheki na RTD palikuwepo mwanamama fulani wakati fulani japokuwa siyo kwa muda mrefu. Naomba ucheki halafu uniambie.

F MtiMkubwa Tungaraza.

 
At Wednesday 12 April 2006 at 14:56:00 BST, Blogger boniphace said...

Hii ni safi sana, kukumbushia historia ambayo tumepoteza. Mija na wachangiaji ninashukuru na kukupongezeni kwa kuendelea kunitajirisha fikra kupitia Gazeti Tando hili.

 
At Thursday 13 April 2006 at 09:41:00 BST, Blogger Indya Nkya said...

Mama wa RTD una maana Eda Sanga? Nadhani alikaimu Ukurugenzi kwa miaka kama miwili

 
At Thursday 13 April 2006 at 10:47:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Ndiyo mzee! Tena wakati RTD ikiwa ndiyo radio pekee inayopeperusha matangazo ndani na nje ya nchi. Ukizingatia na ilikuwa bado ikitumika kama propaganda machine ya itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea, chini ya chama kilichoshika hatamu zote za uongozi!

F MtiMkubwa Tungaraza

 
At Thursday 13 April 2006 at 18:17:00 BST, Blogger MICHUZI BLOG said...

indya umepatia. alikuwa edda sanga na alikuwa akikaimu baada ya mzee abdul ngarawa kustaafu.

mtimkubwa naomba ukumbuke hakuna tena mwanamke alieongoza chombo cha habari chenye tv na redio (serikalini na uraiani) kwa muda mrefu kama joyce mhaville. naomba da'mija umtie kwenye hall of fame yako. ukitaka picha ntakupa

 
At Wednesday 14 June 2006 at 19:00:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Hii ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye hii blog lakini hicho kichwa cha habari kimenifurahisha, so nikaamua na mimi nichangie kidogo ninachokijua ingawaje nimechelewa maana issue hii ilipostiwa 04/06
1962-?? Bibi Titi Mohammed-Deputy Minister for Health, ni mwanamke wa kwanza kuwa elected na MP, wakati huo huo meaning
1962-1965 Bibi Luck S. Lameck(RIP) was Parliamentary Secretary of Co-operatives and Community Development, 1965-1970 ndipo alipokuwa Deputy Minister na 1970-75 akawa Parliamentary Secretary of Health and Social Welfare, shw was one of the first female aliyokuwa elected na MP na hiyo ilikuwa 1961. Asanteni

 

Post a Comment

<< Home