11 March 2006

Aliyenacho ataongezewa...Hii habari imeletwa na Mwanablogu MtiMkubwa. Naomba tuisome vizuri ili tujue kabisa ni wapi tunakoelekea, habari hii hapa chini...

Kuna msemo kwenye maandiko matakatifu ya Biblia unaosema walionacho wataongezewa na wale wenye kidogo watanyang'anywa. Msemo huu unadhihirika sana nchini Tanzania kwa jinsi waliokuwa navyo wanavyoongezewa au wanajiongezea. Siku za nyuma nilipata kutuma ujumbe kuulizia kwamba "..kati ya madaktari na wabunge nani anastahili kulipwa zaidi?.." Niliuliza swali hili baada ya kupata habari kwamba waheshimiwa wabunge walipokutana kwa mara ya kwanza moja ya mambo waliyoyasimamia kidete ni kutaka kujiongezea mishahara. Wabunge walipotaka kujiongezea mishahara wala hawakufukuzwa kazi kama walivyofanyiwa madaktari wa hospitali kuu ya Muhimbili. Suala lao limefunikwafunikwa na umma wa Watanzania haujui hatima ya azima hiyo ya waheshimiwa wabunge. Hii si mara ya kwanza waheshimiwa wabunge kujiongezea mishahara. Mwaka 1975 walipojiongezea mishahara umma haukuridhika. Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakaandamana kupinga azimio la waheshimiwa wa wabunge. Matokeo ya maandamano hayo si kwamba bunge au serikali ilibatilisha ongezeko la mishahara bali iliwafukuza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam!

Kuna baadhi ya mambo yanayonikera sana nchini Tanzania. Mojawapo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ufujaji wa nguvu (abuse of power). Ufujaji wa nguvu unafanywa na wazazi majumbani, walimu mashuleni, viongozi makazini, viongozi wa kisiasa, na walinzi wa usalama wa raia. Polisi, FFU, magereza na wanamgambo ni wafujaji wakubwa sana wa nguvu. Mtanzania wa kawaida akimuona moja kati ya walinzi hawa wa usalama huwa anatishika badala ya kujisikia yupo salama. Walinzi hawa wa usalama wa raia wamejenga tabia ya uonevu na dhuluma zilizokithiri dhidi ya Watanzania masikini. Wiki hii tumeshuhudia walinzi hawa wa usalama walivyoshiriki kwenye zoezi la kuwadhibiti wapiga debe na wafanyabiashara ndogo ndogo kwa amri na ridhaa ya serikali. Matokeo ya zoezi hilo limeua raia wawili na kujeruhi raia na polisi ambao idadi yao hatujaijua.

Binafsi yangu nimeliongelea sana suala la ufujaji wa nguvu za vyombo vya dola dhidi ya wananchi na viongozi wa kisiasa, ndugu, jamaa, na marafiki zangu wengi sana. Nilipata kumueleza kiongozi mmoja wa kisiasa kwamba Tanzania akitokea psychopath kama Foday Sankoh wa Sierra Leone atapata wafuasi wengi sana na upesi sana. Kiongozi huyo wa kisiasa akastuka sana na kuniuliza "..atawapataje?.." Nikamwambia "..wale Wamachinga wanaoonewa, kunyanyaswa na kudhulumiwa na vyombo vya dola ni potential recruits wa rebels katika nchi yoyote.." Akaniuliza "..unafikiri Wamachinga wanaonewa kiasi hicho?.." Nikamjibu "..Si kwamba wanaonewa tu bali wanauawa na wanaichukia sana system!.." Akasema "..una ushahidi wowote?.." Nikamwambia "..Ushahidi wa kwanza mauaji ya Kilombero.." Akanijibu "..Hayo yalishughulikiwa.." Nikamwambia "..Nani alinyongwa kwa sababu ya mauaji ya Wasafwa Kilombero?.. Akanijibu "..Ukifuatilia wapo waliowajibika.." Nikamwambia "..Nina hakika hakuna kiongozi yoyote wa ngazi ya juu aliyefukuzwa kazi kwa sababu ya mauaji yale. Hata mauaji ya Shinyanga waliofukuzwa kazi na kuhukumiwa walikuwa ni watendaji wa chini wa juu walilhamishwa hamishwa na wengine wakarudi na kuwa Rais, Makamu wa Waziri Mkuu, na nafasi zingine za kisiasa!.." Akaniambia "..Hatuzungumzii mauaji ya Shinyanga..Nataka ushahidi kama kuna walinzi wa usalama waliowahi kuua Wamachinga.." Nikamwambia "..Tukifuatilia tutapata ushahidi.." Akaniambia "..Usiseme maneno kama haya yanaweza kukutia matatizoni.." Nikamwambia "..Nisiposema na kukuambia mtu kama wewe ili upelekee kwa wakubwa wenziyo, Mtakuja kustuka siku moja Wamachinga watakaposhika silaha dhidi ya vyombo vya usalama..Mtatahayari siku Watanzania wapole watakapokuwa washenzi kama Wasierra Leone au Waliberia!.." Yale niliyoyazungumza na huyo bwana wiki hii yamekuwa. Tafadhali usichoke kusoma habari kaamili hiyo hapo chini kama ilivyoripotiwa na shirika la habari la Uingereza BBC:

Tanzania suspends street clean-up

Street vendors say moving away from the town centres hits business
A police crackdown on street vendors and bus ticket touts in Tanzania has been suspended for six months after violent clashes left two people dead.
Prime Minister Edward Lowassa said he was halting the operation to allow local authorities and vendors alike more time to prepare for the change.
Vendors and touts have been blamed for a rise in petty crime.
The two deaths occurred on Wednesday in the town of Mwanza along the shores of Lake Victoria in the north.
Four hours of rioting began after police and security guards confiscated vendors' wares and shops and offices in the town were shut down, according to Tanzanian newspaper Mwananchi.
"Many" people were also injured before anti-riot police quelled the violence with tear gas.
Kiosks were also demolished and vendors removed in the capital, Dar es Salaam.
'Adequate preparation'
Mr Lowassa, who originally envisaged completing the clean-up within three months, told the BBC's Swahili service that municipal officials were being given time to plan the clean-up "in a more respectful manner".
With the kiosk's income we could send the children to school and pay for the rent - now we are left with nothing

unnamed street vendor
Vendors facing eviction also needed time to "prepare themselves adequately", he added.
The prime minister said that those traders already moved on would be allowed to continue their business elsewhere because it was the government's policy to "ensure income for everyone".
But vendors complain their new trading spots are not in the town centres and therefore they are being denied their right to a living.
"With the kiosk's income we could send the children to school and pay for the rent," a woman in Dar es Salaam told the BBC as she piled up the remnants of her stand.
"Now we are left with nothing."
The BBC's Vicky Ntetema in Dar es Salaam says the streets of the city looked bare on Friday after the demolitions.
Crimes are often committed in broad daylight in front of the street vendors who do not warn the victims or volunteer information to the police.
Many of the vendors say they were given licenses and paid taxes and they expect compensation from the government for destroying their property.

23 Comments:

At Sunday, 12 March 2006 at 11:23:00 GMT, Blogger MK said...

This comment has been removed by the author.

 
At Sunday, 12 March 2006 at 12:56:00 GMT, Blogger Michuzi said...

naomba nichangie kwa kuwa sina upande katika suala hili, kwani kwa mujibu wa maono yangu, nadhani kila upande unastahili lawama.

nikianza na serikali: hivi kuna ubaya gani kuweka sera ya wazi kuhusu biashara ndogondogo na wafanyaji wake? Kuna ubaya gani kuiga wenzetu ughaibuni kwa kutenga sehemu maalumu za kufanya biashara hizo, na sehemu hizo ziwe zinafikiwa kirahisi na sio kama hivi sasa pale karume ama mwenge. nimeona sehemu kama stockholm wana soko la mchana katikati ya jiji, helsinki pia, berlin nimeona pia hali kadhalika london na johannesburg, kuna masoko ya mchana kwa holoi poloi, lakini hakuna ruhusa kufanya biashara popote kama ilivyo dar, kiasi inatia kinyaa.

Kwa machinga: hivi nani kawaambia kuwa mradi wao walipiga kura kuitia ikulu serikali iliyo madarakani maana yake wafanye watakavyo hata kama ni kinyume cha kanuni? kwa nini wanakuwa wabishi na kuwafanya halmasahuri ya jiji waonekane wanawaonea, kuchoma chipsi na kuuza mashati kila sehemu katikati ya jiji? ni kweli wote wanastahili sehemu kufanyia bizness, lakini ni kila sehemu jamani? mtimkubwa na wengineo hebu rudini muone ilivyo shida kukatiza mitaani dar kutokana na vibanda vya biashara na machinga. sisemi nawachukia,ila kama ni maendeleo yaje kwa nguvu za hoja na sio hoja za nguvu kama anavyotoa mtimkubwa.

nasema haya sababu hata hii serikali imeyaona hayo na ndo maana imesitisha (haijakatisha) kwa muda wa miezi 6 zoezi la safisha jiji, ila baada ya hapo hakuna maslie. lazima barabara iwe barabara na vibaraza viwe hivyo. we umeona wapi chupi zikauzwa kwenye kibanda cha kituo cha basi? sipendi kuweka picha kama hizo bloguni kwani nadhani si vyema kila mtu duniani akaona aibu yetu

 
At Sunday, 12 March 2006 at 15:57:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Muhidin,

Maelezo yako yamenikumbusha fasihi ya kidato cha tatu kitabu cha Ngugi wa Thiongo, This Time Tomorrow. Aibu ya serikali ni kuwa na wauza vyupi katikati ya jiji! Hii mipango ya kuwakarahisha wananchi haikuanza leo: wengi wetu bado tunakumbuka sana halahala za polisi, mgambo, na JKT wakati wa zoezi la kuwahamisha "wazururaji" toka Dar es Salaam kwenda Geza Ulole, Kibugumo, Mwanabilato, Chanika, Chamanzi, Msanga, Mkuranga, Kigamboni na kwingineko koote kwenye makao mapya. Baada ya zoezi hilo likaja zoezi la NGUVU KAZI wananchi wakakarahishwa tena. Akitokea mchunguzi wa mambo ya kijamii (social researcher) kuja kufanya tathmini ya miaka ishirini hadi thelathini baada ya mazoezi hayo sijui kama kutakuwa na matokeo ya mafanikio.

Uchafu kwa fasili yake ni kitu chochote kilichopo mahali pasipohusika. Kama kweli tunataka kusafisha jiji letu kwanza tuanze na kujenga tabia ya usafi miongoni mwetu (personal hygiene). Usafi huu utafanikiwa kwa kuwa kila Mtanzania kujua maana afya bora; kuwa na uwezo wa kula vizuri, kunywa maji safi, kulala mahali pazuri, kuvaa nguo na viatu vizuri, kuweza kununua mswaki na dawa yake. Haya yote yatawezekana ikiwa kama kutakuwa na na uwezo wa kila Mtanzania kuwa na kipato cha kutosha kukidhi mahitaji yake ya kila siku. Kiapto hiki kitapatikana ikiwa tu kama tutaweza kubuni na kuendeleza ajira.

Halafu tukimalizana na suala la usafi binafsi tushughulikie usafi wa mazingira yetu (environmental cleanliness). Uchafu wa mazingira si tu kuwepo kwa Wamachinga katikati ya jiji pia kuwepo mifugo kama kuku, bata, ng'ombe, nguruwe, mbuzi na kondoo katika maeneo ya wanayoishi watu. Nadhani kwa upande wa ufugaji wa wanyama kama ng'ombe, mbuzi, nguruwe na kondoo haupo mitaa ya Kariakoo, Ilala, na Temeke bali Kimara, Mbezi Shamba na Mbezi Beach, Oyster bay, Msasani, Masaki ya Uzunguni siyo Uzaramoni, Kinondoni, Upanga, Sea View, na Mikocheni zote mbili A na B. Hapa ndipo utakapoona aliyenacho ataongezewa. Mkurugenzi wa Jiji ukimshauri atume vijana wake wakabomoe mabanda ya mifugo yaliyopo hizo sehemu nilizozitaja ndipo utakapojua makali na ubutu wake upo wapi.

Hoja ya nguvu na nguvu ya hoja. Nakumbuka katika masaili fulani Bob Marley alisema "..facts 'n' facts is whole lotta o' bullshit.." Wamesitisha na hawakukatisha. Sawa! Kwa nini kabla ya kufikia hatua ya kutekeleza hilo zoezi hawakutathimini mazuri na mabaya yake (pro and cons)? Wanaelimu ya jamii (sociologists), wachumi (economists), au washauri wengine wowote wa serikali wa mambo ya jamii hawakushirikishwa kuitahadharisha serikali juu ya intended consequencies, latent consequencies, na unintended consequencies za zoezi hili?

Rais Nelson Mandela kwenye shajara yake ya Long Walk to Freedom anasema "..ukitaka kuijua serikali nzuri usiangalie inahusiana vipi na raia wake wa juu bali angalia jinsi inavyohusiana na wafungwa wake walio jela.." Haya mambo ya kuikimbiza na kubomoa biashara za watu mijini ni uonevu, unyanyasaji, na dhuluma dhidi ya Watanzania masikini. Kama kweli kuna zoezi la safisha jiji basi lisiwaache na wafugaji wa Oyster Bay, Kinondoni, Ada Estate, Regent Estate, Upanga, Sea View, Mikocheni A na B, Msasani Peninsula/Masaki, Mbezi zote mbili, Kimara, na kwingineko kokote kusikostahili kuwepo mifugo.

Mungu Ibariki Tanzania,

F MtiMkubwa Tungaraza.

KABLA SIJAACHANA NAWE NAOMBA UIMBE KWA SAUTI WIMBO HUU WA MAREHEMU MAKONGORO:

Mpango wa pili wa maendeleo umesema kuleni kuku, mayai, mboga, samaki, maziwa, na kujenga nyumba safi pakulala pawe bora!

HAYA YOTE YATAPATIKANA VIPI SIJUI?

 
At Monday, 13 March 2006 at 04:22:00 GMT, Blogger John Mwaipopo said...

Awali ya yote nilidhani wasafwa wako Mbeya kumbe wako Kilombelo (mchomekeo tu msijali sana)

Pili nichangie kidogo juu ya maslahi ya wabunge na madaktari. Mosi vyombo vya habari vilitupotosha kuhusu hili. Ingawaje sikubaliani na mapendekezo yao ya kutaka kupanuliwa maslahi, vyombo ya habari vilichukulia lile suala kama kikao rasmi ambacho kilikuwa na ansard na minutes. Kumbe yale yalikuwa mawazo ya wabunge binafsi wawili au watatu. Pengine miongoni mwa wabunge wapo ambao walikuwa na mtazamo tofauti. Wanamtandao wakaleta kwetu kana kwamba lile lilikuwa azimio la wabunge woote - Irresponsibe journalism.

Hata hivyo wabunge kama watanzania wengine walikuwa na haki ya walau kuyasema wanayostahiki kuyasema.Madaktari nao walikuwa na haki kudai walichokuwa wakidai. Kosa lao lilikuwa approach. How come wasababishe vifo kwa kugoma kufanya kazi. Ukiwa muhandisi unafikiri kila tatizo linatatuliwa na nyundo. Sivyo. Serikali ilikuwa sahihi kuwaadabisha kama ilivyofanya. Kwa nini hawakutumia power of compromise from different angles. Kizuri hapa hata serikali ilikuwa inatambua madai yao kuwa ni halali. They had no right to cause deaths to innocent and poor patients. Who stopped them from going anywhere around the world to seek greener pastures? Hapa inakuonyesha walikuwa wanatikisa kibiriti tu huku fika walikuwa wanaujua uwezo wa serikali yao.

Michuzi umechambua pande mbili ki ufasaha sana. Huria si holela.Really wamachinga are causing nausea in the 'beautiful' city. Lakini wa kulaumiwa sana hapa ni Serikali, na katu si hawa holoi poloi (asante kwa msamiati huu). Imekuwa iki-react too slowly and unprofessionally. Yenyewe ndio inatakiwa iwe chachu ya uendeshwaji wa shughuli zoote nchini. Mathalani kuhusu suala hili ingeweza kuweka kodi kubwa kwa wafanyabiashara wakubwa wa city centre wanaouza bidhaa sawa na zile za wamachinga. Hii ingewafanya ama waache kufanya biashara hii au ama wafanye kwa asara zao. In the meantime, wamachinga ambao wangetengewa sehemu inayofikika wangeondolewa ama kupunguziwa kodi. Niambie mnunuzi asingeweza hata kwenda mathalani Jangwani (sio kwa Yanga).

Suala ninalolipigia upatu na chapuo bila kusita ni hili alilolileta Mti Mkubwa Mkavu Mnene. Safisha safisha ikirejea ianzie kwa wafugaji wa ng'ombe na mbuzi wa Mbezi beach, Masaki, O'bay na Sea View. Mpango wa kuonea samaki wadogo ufe.

 
At Tuesday, 14 March 2006 at 09:01:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Dada Mija Shija Sayi naomba kuuliza hili swali kwani una miaka mingapi? Je umeolewa? Ktk hii dunia waishi wapi? Je kama ni Tanzania ni mahali gani? Sio Siri kwa sura tu umeumbika je mwili mzima si ndo kabisa! Naomba pokea hii sifa toka kwangu.Nijibu ukipata hili swali.

 
At Tuesday, 14 March 2006 at 18:41:00 GMT, Blogger Mija Shija Sayi said...

Sasa hii mitihani bwana anonymous!

 
At Wednesday, 15 March 2006 at 09:26:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Lakini hiyo mitihani uwa si ina majibu? Mjibu jamaa labda ana mawazo yake? Labda ataka kuoa uwezi jua. Kingine kweli bwana hiyo picha sio mchezo ni kali sana!Tunaomba zile snap za full yaani mwili mzima na sio sura tu. Nasisi twasubiri hilo jibu kwa hamu na tutafurahi kuona picha zako.Tupe ukweli bibie.Bujiku

 
At Thursday, 16 March 2006 at 15:59:00 GMT, Blogger Mija Shija Sayi said...

Bwana Bujiku na bwana anonimasi hapo juu, mnaonaje na kama mngekata shauri la kufungua blogu?...

Karibuni sana katika kusaidia kulisukuma hili gurudumu la ukweli wa papo kwa papo.

 
At Friday, 17 March 2006 at 01:09:00 GMT, Blogger Boniphace Makene said...

Mija hapa umeniacha hoi kabisa...yaani swali la hao unalijibu kisanii kiasi hiki. Ok nimegundua yaani umewapa mtihani mdogo mno maana mahali kwako ni mtu kumiliki Gazeti Tando (natania) lakini raha kabisa na wao wafungue yao kisha waweke picha zao tuwatazame nasi safi hii raha ya blogu ucheshi na utani kidogo na makala za kufichua na kufungua fikra saaaafi sana. Mambo si haya kwa nini Tanzania na Afrika isitanuke na kupata maendeleo. Inawezekana ila bwana anonimasi na Bujiku fungueni Magazeti Tando yenu mtaona matunda yake.

 
At Friday, 17 March 2006 at 15:51:00 GMT, Blogger mark msaki said...

Hoja kali sana Da Mija! ninaufurahia sana ufanyaji kazi wako na tena mnaposhirikiana na Tunga!

nianze na bwana MK usiogope habari ya kufundishwa Urusi. inapokuja suala la living and death, hapo hakuna shule inayotumika. tunapoona nchi zimekuwa na migogoro miaka nenda miaka rudi haina maana kuwa hazikuwa trained kwenye system zake za usalama...unapoongelea suala la amani sijui uko serious au unakoleza mada! hakuna amani kwenye njaa...tuendako ni kwa kuwa makini zaidi maana utandawazi hauruhusu kucheza bao na kupata chakula!! unatoka mzigoni, unapita dukani kununua msosi wa siku hiyo...funga kazi.

Michuziumesema ukweli na umekuwa fair kuongelea pande zote mbili. kuna swali moja waliuliza juzi wana ?DHW "hivi mnakuwa mmejichimbia wapi?" mtu kupandisha maghorofa wakati maafisa wa ardhi wa sehemu husika wapo...... au kuacha watu wajenge vibanda ili uje wafukuze baadaye...hii kimsingi kwa sehemu kubwa huainisha serekali isiyowajibika...

Mti mkubwa ambao ni mkavu ameainisha kila kitu. kurudia ni kujaza ukumbi wa Da mija bure!! kwa kuongezea mimi ninaona ni ajabu kweli kuwa kila mtu anataka kujibanza DAr...mbona hao wamachinga wakionekana mkoani ni dili? kuna kitu si sahihi - (naona Jk ametoa changamoto Arumeru kuwa mikoa ya pembezoni iangaliwe)....

Mwaipopo mengi ya msingi umeyasema..lakini ukiangalia kiundani zaidi, haina maana kuwa ng'ombe anayekupa maziwa zaidi ndio umuhukumu majani kidogo zaidi...reaction ni reaction...sema matokeo yake ndio huwa tofauti..ina maana mfano kama wabunge wangegoma asingekufa mtu...kufa mtu kwa mgomo ni gauge ya kuonyesha kuwa hiyo fani ni sensitive....japo sisemi kuwa nyengine sio, lakini sensitivity hutofautiana. sipingi maslahi ya wabunge, lakini pia siri ya kuwasahau watendaji pia ni ya kujibu....nimeona waheshimiwa wabunge wameliona hilo na juzi walipigia kelele hazina kulikoni na maslahi mabovu!!! myonge mnyongeni lakini haki yake mumpe....ukichunguza sana suala la wabunge na maslahi lilikolezwa na la ishu ya madaktari ambayo ilitugusa wengi lakini tukabaki kuugulia na kulalama.....

Da Mija kichwa inafanya kazi vizuri! Makene upo hapo?

 
At Saturday, 18 March 2006 at 11:46:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Ndugu Mark Msaki sio kwamba naogopa kufundishwa Russia bali hii ndio facts ambapo ukweli wake utaoneshwa pale hilo tukio likitokea.

Vyanzo vya ulinzi vinavyolinda Taifa hili vina macho makubwa ndani ya nchi na nje ya nchi sasa sijui hizo silaha utazipitisha wapi kufanya mapinduzi hayo?

Au wananchi kutumia silaha za jadi ambapo watatwaa eneo gani na kusema ndio nchi wamechukua?

Wanajeshi wetu wapo tayali ktk matukio kama hayo ambapo narudia tena nina uhakika wa zaidi ya asilimia mia mbili (200) yatazimwa chini ya masaa 24.
Nadhani bwana Michuzi atakuwa na marafiki zake wengi wa namna hii (wanao linda taifa hili ndani ya nchi na nje ya nchi) ambapo ukiwauliza watasema kama ninavyosema.(Inategemea maana kazi hii ni kama mtoto, unakula kutokana na umri wako = Unajua mengi kutokana na nafasi yako na kitengo chako)

Mataifa mengi ya Africa unayo yaona yana matatizo ya Vita, Sio kwamba Vita hiyo imeanzishwa na mtu mmoja bali imeanzishwa ktk kushirikiana na Mataifa mengi zaidi ya Africa na ya nchi za nje kwa kudhaminiwa kipesa, wanajeshi (watu kufundishwa na ata kununua au kukodisha wanajeshi wale waliostaafu kutoka ktk Mataifa mengine mengi ya Africa), silaha n.k.

Naomba angalia hili swala kwa undani zaidi utaona ninayo sema.
Mfano: Sir Mark Thatcher na mataifa mengine yaliyotaka kuleta mapinduzi Equatorial Guinea lakini kutokana na Good Intelligence report iliyopatikana kutoka kwa mataifa mengi mbalimbali ya Africa yaliweza kutoa habari kwa Serikali za South Africa,Equatorial Guinea,Zimbabwe, na mengi yaliwezesha kwa Sir Mark Thatcher na wenzake wote kukamatwa na mapinduzi kuzimwa kabla ya kutokea.

Sasa Tanzania tuna macho ya kuona Adui kama Binadamu na Adui kama Taifa lolote litakalo kuwa na mawazo ya kupindua nchi yetu na pale tunapofahamu tunazima hiyo mission yao kabla ya tukio kutokea.

Ndio maana ninakwambia Taifa letu kutokea mapinduzi ni vigumu sana, Hii sio kwamba ninazungumza kufurahisha jamii au kukoleza mada la hasha ninazungumza kwa kile ninachokijua kwa undani zaidi.
Tanzania ni moja ya mataifa ya Africa yaliyokuwa na watu waliokuwa na mafunzo ya namna hii (ya hali ya juu) pamoja na jinsi ilivyotawanya macho yake ktk kulinda Taifa hili Kubwa la baadae ulimwenguni.

Mwisho, Vita zote unazoona Congo, na mahali popote pale Africa ni mikono ya Mataifa mengine ya Africa, Mataifa mengine nje ya Africa kupitia raia wa ndani wa nchi husika na wakimaliza wanachotaka toka kwako (Interests kuisha) wanakuua au ku-support mtu mwingine na Vita inaendelea tu upya.

Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

Nashukuru.
©2006 MK

 
At Wednesday, 22 March 2006 at 14:15:00 GMT, Anonymous ndesanjo said...

Kuna jambo Mti kasema aliulizwa na ofisa wa sirikali. Ofisa huyo alitaka ushahidi wa unyama na ukiukwaji wa haki za binadamu. Watwawala wetu wanapenda sana kukimbilia hilo neno, "ushahidi." Mkapa kuna wakati aliviambia vyombo vya habari/uongo vitoe ushahidi kuwa sirikali yake ina wala rushwa. Kitendo cha kiongozi wa sirikali kutojua kuwa vyombo vya dola Tanzania mara nyingi hunyanyasa wananchi na haki za msingi hukiukwa bila woga wowote kinaonyesha kuwa huyo bwana anatakiwa aongozwe na sio aongoze. Hata Mkapa nilimshangaa sana...rais mzima hajui kuwa amezungukwa na wala rushwa anataka wandishi wa habari wampe ushahidi. Keleuwii!

 
At Friday, 24 March 2006 at 15:16:00 GMT, Blogger msangimdogo said...

Lakini hii si ndio Bongo jamani??

 
At Sunday, 26 March 2006 at 07:37:00 BST, Anonymous Anonymous said...

MK,

Nashukuru sana kwa maoni yako.

Imani ya kwamba pale nyumbani pako salama na pana walizni ni nzuri lakini tusilale mlango wazi. Nina maana hata kule kwenye vyombo vya usalama vyenye nguvu na ujuzi kuliko vyetu imewezekana kufanya matendo ya kigaidi na kuingizwa silaha! Kwa mifano hai ni September eleventh, milipuko ya mabomu ya IRA, milipuko ya mabomu Israeli, Moscow, Madrid, Ufaransa na kwingineko sembuse Tanzania ambako kitengo cha makonteina bandari kimebinafsishwa pia tumezungukwa na vita Uganda, Burundi, na Kongo. Kongo inaweza kuwa bonge la kichochoro cha kupitishia silaha kuingia Bongo!

Audhu billah hima shetani rajimu, Allah karim! MUNGU ilinde Tanzania.

F MtiMkubwa Tungaraza.

 
At Sunday, 26 March 2006 at 15:20:00 BST, Blogger MK said...

This comment has been removed by the author.

 
At Monday, 27 March 2006 at 15:31:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Mk,

Asante kwa ujumbe wako.

Awali kabla sijaendelea sana naomba unielewe kwamba nilichozungumzia siyo mapinduzi au machafuko nchini Tanzania. Nilichozungumzia ni tahadhari juu ya kutengeneza watu watakaoweza kuwa waasi kwa sababu za kisiasa, kijamii, na kiuchumi.

Kwa kifupi tu mimi ninafanyakazi na watu waliotoka nchi zilizoathirika na vita. Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana sababu zilizosababisha vita nchini kwao na nani wanaoshiriki katika kupigana vita. Kwa ufupi huwa wananiambia vita vyote vinatokana na kupunjana kiuchumi, tofauti ya itikadi za kisiasa. Pia kwa sababu za kijamii kama ukabila, dini, na rangi. Halafu kuhus kina nani wanaoshiriki kupigana vita huwa wananiambia ni wavulana na wanaume vijana wasio na kazi na wenye elimu ya chini na wanaume wenye umri wa makamo kati ya miaka 35 na 45!

Jingine, ulipozungumzia Chechnya kuna suala zaidi ya kuipunguza Urusi nguvu. Chechnya ina mafuta. Jinginewe zaidi Mchechnya na Mrusi ni watu tofauti wenye dini, lugha, na tofauti zingine za kiutamaduni. Wahusika wakuu wa vita hivi ni Wachechnya wenyewe wakisaidiana zaidi na Waislamu toka nchi za Kiarabu.

Halafu kuhusu Museveni na ndege za kijeshi sina hakika nalo. Lakini sidhani kama katika maadili ya kivita kama anaruhusiwa kutumiwa ndege kupigana LRA.

Halafu suala la Dubai Ports World limesitishwa. Kwa hiyo bado hawajaanza utendaji. Nakuomba fuatilia tena au kama mimi ndiyo sina habari kamili naomba unijulishe.

Halafu unaposema Burundi vita imekwisha na kwamba kuna vikundi vidogo vidogo tu hiyo ina maana vita bado ipo. Sijui fasili nzuri ya vita kwa Kiswahili lakini kwa Kiingereza naweza kusema War is a fight for the gain based on right or wrong reason/s. Mwanamuziki Gill Scott-Heron katika wimbo wake Work for Peace anasema "..Peace is not absence of war. Peace is even the absence of rumours of war.." Kwa hiyo pasipo amani pana vita.

Nisikuchoshe sana bali nakuomba usome tena waaraka wangu. Niliposema Burundi, Uganda na Kongo wanaweza kuwa vichochoro vizuri sana kwa wenye nia ya kuleta mabaya nchini mwetu. Sikusema Burundi inaweza kupigana na Tanzania. Jinginewe tusijisahau sana tukafikiri sisi wakubwa sana. Mtanzania aliyempiga Idd Amin siyo Mtanzania wa leo. Mtanzania yule alikuwa na dhana ya Utanzania chini ya itikadi ya Ujamaa ambayo ilikuwa inamgusa kila sehemu ya maisha yake ya kila siku kuanzia gazeti la UHURU/MZALENDO na DAILY NEWS/SUNDAY NEWS, Idhaa ya Taifa, Biashara na External Service za Radio Tanzania Dar es Salaam. Usafiri wa KAMATA na yale ya mikoa CORETCO, MORETCO na mengineyo, UDA, Reli ya Kati na TAZARA. Wakati ule palikuwa na umoja wa Kitaifa miongoni mwa Watanzania sasa hivi umoja huo umelegea sana kwa sababu ya kutokuwa na itikadi wala sera za kitaifa ya kitaifa. Kuwajibika, Ukweli na Uwazi, Ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya siyo sera wala itikadi hizi ni kauli mbiu ambazo hazijengi uzalendo wala utaifa.

Mungu Ibariki Tanzania.

 
At Tuesday, 28 March 2006 at 10:08:00 BST, Blogger MK said...

This comment has been removed by the author.

 
At Tuesday, 28 March 2006 at 13:19:00 BST, Anonymous Anonymous said...

MK,

Ninafurahi kubadilishan mawazo nawe. Ninafurahi kuwa una imani kubwa sana juu ya vyanzo vyetu vya ulinzi. Hapa nina maswali kadhaa "..Hivi kama kweli vyanzo vyetu vya ulinzi ni kiboko namna hiyo silaha wanazotumia majambazi zinaingiaje nchini? Pili, vinashindwaje kudhibiti matukio ya ujambazi, uingizaji na upitishaji wa madawa ya kulevya kwa mfano makonteina ya mihadarati yaliyokamatwa Romania, na utoroshaji mali kwa mfano makonteina ya mchanga wa dhahabu bandari ya Tanga.."

Halafu ajira katika jeshi, polisi, mashirika na makampuni zinahitaji qualifications za kitaaluma na jeshini na polisi pia wajihi. Tukumbuke kwamba mwekezaji Tanzania hajafungua makampuni yanayohitaji harubu(manual labour)! Kwa hiyo vijana wasiyo na elimu hawahitajiki kwenye uzalishaji mali na utoaji huduma. Wengi wa wawekezaji wamewekeza kwenye rasilimali za asilia kama madini, mbuga za wanyama, na huduma za jamii kama mabenki, mahoteli, usafiri wa anga, na majini. Ardhini hakuna mwekezaji atayejipinda kuwekeza kwenye usafiri wa mabasi au kukarabati na kuboresha huduma reli ya kati, sana sana wanaitamani reli ya TAZARA ambayo kwa mikataba yake hatuwezi kuibinafsisha. Hapa naomba unipe taarifa za kweli(facts) mpango/mipango ya/wa serikali wa kuboresha na kukuza ajira kwa vijana. Wiki iliyopita nilijibu ujumbe kutoka kwa jamaa yangu mmoja aliyeniuliza kuhusu "..mafanikio ya mpango wa maji safi kwa wote ifikapo mwaka 2000.." Ninatumaini hili suala la ajira kwa vijana halitakuwa kama la mpango wa maji safi kwa wote ifikapo 2000.

Kuhusu hali ya usalama Zanzibar hilo ni jambo linlohitaji mikakati ya kweli. Kwa sababu makovu na vidonda vya vilivyosababishwa wakati wa utawala wa sultani, machafuko na mauaji wakati wa uchaguzi wa mwaka 1963/4, mapinduzi ya Januari 1964, machafuko ya 1972 na mauaji ya Hayati Sheikh Abeid Aman Karume, machafuko na mauaji ya Januari 2000 makovu na madonda haya bado mabichi miongoni mwa Wazanzibari.

Mshairi maarufu wa Kiayalendi William Butler Yeats katika shairi lake la The Second Coming alisema

"...Turning and turning in the widening gyre
The falcon cannot hear the falconer;
Things fall apart; the centre cannont hold;
Mere anarchy is loosed upon the world,
The blood-dimmed tide is loosed, and everywhere
The ceremony of innocence is drowned;
The best lack all conviction, while the worst are full of passionate intesity.."

MK, the Second Coming yaweza kuja popote ulimwenguni. Watanzania kama wanaulimwengu wengine wowote hatuna sababu ya kufikiri kwamba Second Coming kwetu haiwezi kuja. Kuna msemo jihadhari kabla ya hatari ambapo kinyume cha msemo huo ni kwamba mwenziyo akinyolewa wewe tia maji. Watanzania tuna nafasi kubwa ya kuchagua kati ya jihadhari kabla ya hatari au mwenziyo akinyolewa wewe tia maji.

Mkweli kwa nchi yangu,
F MtiMkubwa Tungaraza.

 
At Tuesday, 28 March 2006 at 14:23:00 BST, Blogger Michuzi said...

da mija mbona umekuwa mvivu? kila siku nachungulia naona hamna tarehejuu. ni aje? salaam zako kwa kibiriti, mbunju na teddy zimefika. wote wanahoji kurudi kwako... pia niulizie makene nani kapitisha jina gazeti tando? ana agenda gani kila kukicha gazeti tando...gazeti tando

 
At Tuesday, 28 March 2006 at 19:06:00 BST, Blogger MK said...

This comment has been removed by the author.

 
At Tuesday, 28 March 2006 at 21:45:00 BST, Blogger Mija Shija Sayi said...

Michuzi asante kwa kunikumbuka, wakati mwingine mambo huingiliana sana hadi kujikuta unatoweka sehemu moja, lakini kuanzia wiki ijayo nitarudi na kasi mara mbili.

Hili suala la Gazeti Tando hata na mimi bado najiuliza..."Makene taratibu jamani...
...............................

Kaka zangu MK na MtiMkubwa, natafuta namna ya kuuweka huu mjadala hadharani maana ni wa aina ya pekee.

Tuko pamoja.

 
At Thursday, 30 March 2006 at 14:21:00 BST, Blogger msangimdogo said...

Damija kazi kweli unayo, sikuwa nimepitia maoni ya yule jamaa aliyeomba akuone mzima na wala sio sura tu, lakini pia nikafurahishwa sana na jinsi mjadala ulivyolakizika.....Mnajua nini ndugu zangu? Ni lazima watu wa aina hii wawepo duniani ili kupafanya mahali bora pa kuishi

 
At Saturday, 1 April 2006 at 03:47:00 BST, Anonymous mtandawazi said...

Nilidhani dhambi hi ina wabunge wakenya tu, kumbe ni ugonjwa unaoambukiza kila mwenye madaraka..Nimejaribu kufafanua wabunge wakenya wanavyonyonya raia katika blogu yangu

 

Post a Comment

<< Home