17 July 2005

...labda Yesu amepotea...!!!!

Majuzi, mwanangu Shija,(mtoto wa dada yangu)mwenye umri wa miaka tisa aliniacha hoi, ilikuwa ni jioni, mvua kubwa iliyoambatana na radi kali za mwanga na kuunguruma ilikuwa ikinyesha. Shija alikuwa kimya akiangalia dirishani, nilidhani kwamba anaangalia jinsi mvua inavyonyesha kumbe alikuwa na fikra zake, akaamua kutoa duku duku lake...

Shija: (akiniita) Mam'dogo Mija....

Mija: Unasemaje?

Shija: Labda Yesu amepotea mbinguni...

Mija: (Kwa mshtuko na ka mshangao kidogo) Hee! kwa nini unafikiri hivyo??

Shija: Kwa ajili ya hizi zinazopiga (radi)...Labda yesu amepotea sasa wanamtafuta...

Mwanangu huyu aliniacha mdomo wazi, nikabaki daa! huku nikifikiria nianzie wapi kumpa somo. Lakini pia nilijifunza kwamba si kila mtu huwa na fikra moja juu ya jambo fulani ambalo liko wazi na linalojieleza. Na vile vile niligungua kwamba kama unataka kupata mtazamo mpya juu ya jambo fulani, basi waulize watoto kwani wenyewe husema hasa lile wanalolifikiria kuwa ndilo, lakini watu wazima mara nyingi husema yale ambayo wanadhani watu watafurahi kuyasikia, hata sijui ni kwanini watu wazima tuko hivi?? Hili jambo nitalizungumzia hivi karibuni...ngoja nikikimbilie kitanda.

9 Comments:

At Sunday, 17 July 2005 at 14:44:00 BST, Blogger Indya Nkya said...

Kaongea hasa alichosikia. Si unajua tunaambiwa mbinguni ni juu? Yesu tunaambia atakuja akitokea mawinguni. Huyu mtoto kaa naye karibu na ongea naye anaweza kukusaidia mengi.

 
At Tuesday, 19 July 2005 at 14:23:00 BST, Blogger Reginald S. Miruko said...

Nimefurahi kupata story ya mwanao huyo. lakinbi wanasaikolojia wanasema kuwa mtoto anapozaliwa huwa kama karatasi nyeupe (isiyoandikwa) na mawazo (maandishi) hupatikana kulingana na mazingira yanayomzunguka. Usishangae hata chembe, mtoto huyo amepata mawazo kwenye familia yenu au majirani kuwa 'Yetu atarudi', ndipo akajenga taswira ya kupotea, la sivyo asingeweza.

 
At Thursday, 21 July 2005 at 08:20:00 BST, Blogger msangimdogo said...

Laiti kila mtu duniani angekuwa na utashi wa watoto, basi sio ajabu kuwa dunia ingekuwa sehemu ya amani na hakika ingekuwa pepo kwa maana kila mmoja angelikuwa anatoa kile anachohisi yeye sio kuwafurahisha wengine.

 
At Friday, 22 July 2005 at 11:10:00 BST, Blogger Indya Nkya said...

Msangi kasema ukweli watoto ni wanafikra huru hawajaaribiwa na ushenzi wa dunia hii. Kuna siku nilikuwa uwanja mmoja wa ndege nikisubiri muda wangu wa safari. Kulikuwa na watu wengine kadhaa akiwepo mtu mweusi na mtoto wake, mtu toka asia na mtoto wake na mzungu na mtoto wake. Wakati wazazi wao wote wakiwa wanajifanya kusoma ama kitabu au gazeti, watoto wao walijikuta wakicheza pamoja kwa nguvu zote bila kujali chochote. Wazazi walibaki kila mmoja akimwangalia mwanae. Pengine kila mmoja alikuwa akilaani mtoto wake kucheza na mtoto wa rangi tofauti. Sikuona hawa wazazi wakizungumza kati yao kabisa lakini watoto walicheza hadi muda wa kuondoka ulipowadia

 
At Wednesday, 27 July 2005 at 10:48:00 BST, Blogger Martha Mtangoo said...

Malezi jamani nayo pia yanachangia, hebu fikiria mtoto angezaliwa katika familia ambayo baba anatoka alfajiri anarudi usiku wa manane, mama naye ndo usiseme anatoka usiku anarudi usiku mtoto hajui hata aendelee kuishi kwa style gani, lakini kumbe amelelewa na baba na mama na akila siku anaenda kanisani kumbe anajua kuna mtu anaitwa Mungu na Mungu ana mtoto wake anaitwa Yesu na Yesu ana mama yake anaitwa Mariamu, na ipo Siku atarudi hapa Dunian! inapendeza sana. Mleeni kwa utamaduni huo alionao na si Vingine.

 
At Wednesday, 27 July 2005 at 10:59:00 BST, Blogger Martha Mtangoo said...

Ni malezi tu hayo endeleeni kumlea zaidi hapo mtaona wenyewe atafanya maajabu halafu ahapo baadaye ataitwa Profesa, huo ni ubunifu wa Mtoto.

 
At Sunday, 7 August 2005 at 22:05:00 BST, Blogger Ndesanjo Macha said...

Da' Mija, mzima?

 
At Friday, 12 August 2005 at 10:44:00 BST, Blogger kivale said...

nimtazamo wake katika yaleanayo jifunza kutoa kwa wanadamu kwa yale wanayosema na kutenda.hayo yanajiludia katika kichwa chake

 
At Friday, 2 September 2005 at 18:54:00 BST, Blogger Ndesanjo Macha said...

Da,
Ukipotea kweli unapotea!

 

Post a Comment

<< Home