"Unapokuwa mwanamke mweusi duniani..." Hotuba aliyotoa Winnie Mandela Chicago Marekani.
Mwezi uliopita Winnie Mandela kwa heshima zote alialikwa na jamaa wa V-103'Expo huko nchini Marekani (Chicago) kuhutubia juu ya Nafasi ya mwanamke mweusi duniani, Winnie aliandaa hotuba nzuri sana lakini tofauti na matarajio yake watu waliacha kumsikiliza na kwenda kuangalia maonyesho mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika ukumbi huo na yeye kutokana na utovu ule wa nidhamu akaamua kukatisha hotuba.
Ni hotuba nzuri na sana nimeona niwawekee hapa ili wote tuisome. Mwandani asante kwa kuniletea habari hii nimeona si bora kuifaidi peke yangu.
5 Comments:
da mija mbona anna tibaijuka unamsahau?
Michuzi, sijamsahau Tibaijuka unaweza kumpata hapa http://damija.blogspot.com/2005_11_01_damija_archive.html
Da Mija, safi sana kutupa hotuba hii. Kazi za kutunza hizi.
Yes,
Nimekuwa napitanapita hapa kila mara nikiwa na wingi wa mawazo na maoni lakini kuna kitu kinanizuia sana kuandika mawazo na maoni yangu juu ya hili.
Mawazo na maoni yangu juu ya hili yalielekea moja kwa moja katika kuwapima kwenye mzani kina mama wa kariba ya Muheshimiwa Winnie Mandela kwenye medani ya kisiasa. Ungekuwa karibu ningekuuliza kati ya Winnie Mandela na Golda Meir nani anastahiki na kustahili kuzomewa na kubezwa? Au zaidi, kati ya Winnie Mandela na Magreth Thatcher nani anayestahiki na kustahili kuzomewa na kubezwa?
Na hata hii leo kati ya Winnie Mandela na Condoleza Rice nani anastahiki na kustahili kuzomewa na kubezwa?
Zaidi ya hivyo, ingewezekana kumsilimisha Winnie Mandela kwa yale yote awayo na kuwa mzungu, ninasema bila woga wala kusita Winnie Mandela angekuwa shujaa na angejengewa minara, na angenakshiwa kwenye sarafu na noti, na kutungiwa vitabu, na kuzungumzwa kwenye mabaraza mbali mbali yenye heshima na taadhima, na kufundishwa kwenye taasisi za elimu tangu vidudu mpaka vyuo vikuu! Leo siye kwetu Afrika tena kwa ridhaa ya mumewe na chama chake cha ANC na wengine wote waliohusika shujaa huyu kageuzwa muhuni na mwanamke asiye na maana.
Ningesema sana lakini naishia hapa,
F MtiMkubwa Tungaraza.
MtiMkubwa Tungaraza, umenena, Winnie Mandela, ni shujaa. Huyu mama hana mfano. Mzee Mandela, alikumbwa na matatizo ya wanaume wa kiafrika. Ukisoma historia ya familia ya Mandelas, utagundua kwamba Mama Winnie, ni shujaa na anastahili sifa nyingi.
Siku nyingine nitawamegea sifa za mama huyu ambaye waliowengi wanamchukia kwa vile aliachana na Mzee Mandela. Mzee Mandela, naye si mtakatifu, ana mapungufu yake kama binadamu.
Da Minja, asante kutuletea habari za Mama Winnie na wanawake wengine mashujaa wa Afrika na Dunia nzima.
Ni,
Padri Privatus Karugendo.
Post a Comment
<< Home