14 April 2006

Bibi Mohamed!..Mwanamke wa kwanza nchini kushika madaraka ya uwaziri. Hongera MtiMkubwa kwa kutegua.




Kwanza niwashukuru wachangiaji wa mada hii, na pia tumpigie makofi ya pongezi MTIMKUBWA Tungaraza kwa kutegua kitendawili hiki mapemaaa! Huyu jamaa ana kumbukumbu za karne. Pia ninamshukuru bwana Michuzi kwa kuibua mjadala mwingine juu ya kina mama na uongozi katika vyombo vya habari, binafsi nilikuwa bado sijaanza kuifuatilia nyanja ya Habari na nafasi ya wanawake katika kuviongoza vyombo hivyo..."Raha ya blogu jamani".

Haya, Bibi Titi Mohamed alikuwa si mwanamke wa kwanza tu kushika nafasi ya uwaziri nchini, bali pia ni mwanamke wa kwanza aliyejitolea kupigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana bila kukata tamaa pamoja na kwamba alikubwa na misukosuko mingi. Hapa kuna habari kamili ya jinsi alivyojiunga na harakati hizi za ukombozi. Habari hii aliitoa yeye mwenyewe miaka michache kabla ya kufariki kwake. Na hapa kuna orodha kamili ya mawaziri wanawake wa Tanganyika na Tanzania.

Shujaa Bibi Titi alifariki 5/11/2000 katika hospitali ya NETCARE Johannesburg Afrika Kusini.

7 Comments:

At Friday 14 April 2006 at 12:00:00 BST, Blogger mzee wa mshitu said...

Da mija

Safi kwa kutupa changamoto ya kukumbuka historia yetu, lakini mbona katika hiyo orodha ya mawaziri wanawake wa Tanganyika- Tanzania kuna dosari kwa mfano katika miaka ya 1982-88 wameonyesha kuwa Naila Lazaro Kiula alikuwa Naibu Waziri wa Elimu wakati yeye ni mwanamume.

Hivyo pamoja na orodha yao kuwa nzuri hapo imetia dosari.

 
At Friday 14 April 2006 at 14:46:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Halafu jingine Damija, ni kwamba hata kabla ya Bibi Titi Mohamed kuingia kwenye harakati za ukombozi walikuwepo wanawake wengine kwa mfano aliyekuwa Mtemi wa Waha Mwami Theresa Ntare ni mmoja kati ya wanawake wa shoka Tanzania.

f MtiMkubwa Tungaraza.

 
At Friday 14 April 2006 at 18:51:00 BST, Blogger MK said...

This comment has been removed by a blog administrator.

 
At Friday 14 April 2006 at 19:47:00 BST, Blogger espionage said...

This comment has been removed by a blog administrator.

 
At Friday 14 April 2006 at 20:04:00 BST, Blogger John Mwaipopo said...

Mija kwa kusakanya-sakanya masuala sikuwezi. Hongera.

 
At Wednesday 19 April 2006 at 18:58:00 BST, Blogger MICHUZI BLOG said...

damija kuna afande madawili naomba ucheki naye. yeye ni brigedia na mwanamama mwenye cheo cha juu kuliko kinamama wote jeshini. picha yake ntakutumia

 
At Thursday 27 April 2006 at 15:56:00 BST, Blogger Chesi said...

Cherahani umeniwahi, na mimi nilitaka kusema hivyo hivyo. nadhani Da mija alikuwa na maana ya mzee wetu wa siku nyingi Nalaila Kiula ambaye katika miaka miwili mitatu ya karibuni amekuwa akisumbuliwa sana na kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu pengine baada ya kuwa 'si mwenzetu' tena!

Halafu Mija, naomba uangalie tena kumbu2 zako maana mimi za kwangu zinaniambia kuwa Sigela Nswima alikuwa ni waziri mwanaume....

naomba pia uangalie jina la huyu Fay King Chung maana kama sijakosea katika kipindi hicho hii TZ ilikuwa haina waziri wa kike mwenye jina hilo......ni orodha nzuri, lakini.

 

Post a Comment

<< Home