09 May 2005

Hivi tumerukwa.....??

Kuna jambo moja ambalo mara nyingi silielewi, hivi ni kwa nini waafrika tulio wengi tumekubali kujishusha namna hii? kiasi kwamba tunawasaidia wenzetu hawa weupe kuwapa chati bila woga hata kidogo. Majuzi nilikuwa na rafiki yangu tukitembea mitaani, kwa kweli mitaa tuliyokuwapo hairidhishi kiusafi hata kidogo, vinyesi, harufu na ramani za mikojo kutani, makaratasi yamesambaa ovyo, na mengine mengi. Rafiki yangu akaanza kwa kuguna..mh! utadhani tuko Afrika...hataa hii si bure lazima sehemu hii wakazi wake ni watu weusi, nikamuuliza kwa nini unasema hivyo, ina maana yaliyo mazuri yote ni ya wazungu na mabaya yote ni ya waafrika? akasema bwana eeh, hawa wenzetu wametuacha sana, hata iweje hatutakaa tuwapate....Hakyanani niliishiwa la kusema ila nikamkumbusha usemi usemao 'usipojidhamini ni nani atakuthamini?'

Hali hii imenikumbusha tabia ya waafrika walio wengi waishio ughaibuni kutokutaka kupiga picha kabisa katika maeneo mabovu mabovu, utasikia wanasema, watajuaje kama niko majuu bwanaa?? piga picha hata ukipeleka kwenu picha yenyewe inajieleza.
Jamani tubadili tabia hii, ni lazima ukweli uwe ukweli kwani kwa tabia hii tunajishusha wenyewe na kuwapandisha wenzetu, mbona wenyewe wakija kwetu wanakwepa kupiga picha mambo mazuri?? tujiulize hilo...ukweli bado uko pale pale si maeneo yote ya ughaibuni ni mazuri, na si maeneo yote ya Afrika na mabovu.

MKOMBOZI WA MWAFRIKA NI MWAFRIKA MWENYEWE.

2 Comments:

At Tuesday, 10 May 2005 at 09:42:00 BST, Blogger Indya Nkya said...

Da Mija safii na karibu kwenye ulingo. Soma makala yangu niliyoandika kuhusu utamaduni wa amani nimegusia hilo suala la kuthamini wazungu. nenda kwenye blogu yangu inaitwa pambazuko.blogspot.com

 
At Wednesday, 11 May 2005 at 04:09:00 BST, Anonymous Anonymous said...

Jina la kitu unachoongelea ni utumwa wa kimawazo. Kituo!

 

Post a Comment

<< Home