Utukutu wa chama.
1. Chama chetu kimetuongoza, hadi uhuru tulipoupata,
Kinaendelea kuongoza, kufikia lengo umoja,
Mwenyekiti Mwalimu Nyerere, mwenye hekima na wingi wa sifa,
W: Tanzania.
Ewe chama chombo chetu madhubuti kabisa,
Ndio wewe nguzo, muokozi wa taifa,
Mwenyekiti Mwalimu Nyerere mwenye hekima na wingi wa sifa,
W: Tanzania.
2. Kwa wasafiri wenye busara, ni wajibu wao kukumbuka,
Wafikapo safari salama, hata njiani bado wakiwa,
Kulinda chombo chao vyema, pia nahodha kumshikilia,
W: Tanzania
3. Ulifika wakati mgumu, wananchi walifadhaika,
Utumwa ukoloni ni sumu, sisi sote tulihangaika,
Ni wajibu wetu kushukuru, Nyerere alipojitokeza,
W: Tanzania.
4. Chama chetu kweli ni ngome ya chuma, sisi sote tunazingatia,
Mwalimukiongozi wa umma, nani twaweza kumlinganisha?
Ametutoa katika utumwa, wananchi sasa tnalinga.
W: Tanzania.
NCHI YANGU ENZI HIZO...
4 Comments:
Sasa ondoa hilo neno utukufu weka "utukutu" wa chama.
ulicheza halaiki we?
kweli umekuwa "malenga" wetu sasa!
kwakweli kama alivyosema Indya, hakika unatakiwa kusahau kabisa matumizi ya hilo neno Utukufu maana umebaki Utukutu hivi sasa
Post a Comment
<< Home