Ngo...ngo...ngo..hodiii!
Ngo...ngo..ngo... hodiii, jamani wenyewe mpoo?...inaelekea wametoka, ngoja niache ujumbe mlangoni. Wanablogu, Nilipita kwenu lakini inaelekea hamkuwepo, nia hasa ilikuwa nikuwapa taarifa kwamba nami nimeingia katika ulimwengu wa blogu. Blogu yangu itajulikana kwa jina la Da'Mija, Da mija atakuwa akizungumzia masuala ya jamii na mabadiliko yake ya kila siku. Atafundisha atakapoona panafaa kufundisha, atajadili pale atakapoona panafaa kujadili, atatoa mawazo pale atakapoona panafaa kutoa mawazo na mengine mengi yatajitokeza kulingana na siku zitakavyokuwa zikienda. Asanteni. |
8 Comments:
Karibu mwanakwetu!!!!
karibu sana , nasi tunasubiri kwa hamu kusoma mengi kutoka kwako
Tunasubiri dada Minja usaidie katika jitihada za kuhabarisha jamii hasa wakati huu wa kujenga jamii habari
haya ni mafanikio makubwa sana kwa wanawake wa Kiafrika ambao wanaanza kuona umuhimu wa kudhihirisha utamaduni wao na kujivunia popote waendapo. Karibu, karibu dada
Mh! umegonga kwa kasi sana kiasi tukaogopa kuwa tumevamiwa, si unajua tena watu walivyokata tamaa kuibuka na kukupiga roba za mbao sio jambo la ajabu kwahiyo mgeni akigonga lazima usikilizi anavyogonga kama anatumia FATUMA au laa. Karibu sana sisi tupo, karibu mgeni
Duuuu.... karibu mshirika ndo mambo hayo tunayotaka toka kwa ma dada zetu... Karibu Saaaana!
Da' Mija,
Hongera sana!
Fidelis Tungaraza.
nakushauri kuwa uweke kitabu cha wageni ndugu yangu
Post a Comment
<< Home