Eti siku ya mtu kuzaliwa ni ya nani?..mama au mtoto?
Pichani juu ni mimi na kaka yangu na chini ni mzaa chema.
Hapo kipindi cha nyuma nilipata kuzua mjadala na mshairi maarufu wa kikundi cha Parapanda Mgunga mwa Mnyenyelwa juu ya hasa ni nani mwenye haki ya kuiita siku yake, je ni mama au mwana? kwa mujibu wa Mgunga anasema siku ya mtu kuzaliwa ni haki ya mama na kama ni sherehe au pongezi zote anayetakiwa kupewa ni mama. Hili nimelikumbuka leo kwa vile ni siku yangu ya kuzaliwa..., haya wewe unasemaje? ni nani anayetakiwa kupewa pongezi katika siku za kuzaliwa?
11 Comments:
hepibethdei tu yuuu...X 3
hawoldayunaaauw....X 3
heeepiiiibethdaytu yuuuuuuu...X 1
jana tumesherehekea muungano, na hatukuwasherehekea nyerere na karume. mi nadhani bethdei ni siku ya mtoto...
Naunga mkono kwamba siku hiyo ni ya mtoto.Mama alishawahi kupata yake kutoka kwa bibi wa mtoto.Ni siku ya mtoto.
siku ni ya mtoto. Haswa kwa vile naona baba kasahauliwa. Mama na baba siku yao ni ile ilipotungwa mimba, au?
Hepi bethidei tu yu. Siku ni yako.
Happy Birthday Damija! May God gives You 100 Years and more in Life.
Thanx,
©2006 MK
WOW what a wonderful picture,Happy birthday to you Damija. Siku kwa hakika ni ya mtoto, mama atasherehekea nini wakati yake yamepita,au Mgunga anataka kusema mama anapojifungua anakuwa anazaliwa upya, sidhani. Ciao Happy to you!
Mija;
Ikalaga na Mhola na Mulungu Agwinhe lubango lutaale uje gubutongi na buyegi bo shiku joose.
Nsizayo Ng'wanamatondo
Heri ya siku ya kuzaliwa Da Mija. Uwe na maisha marefu (iwapo utakuwa unakula vizuri, kufanya mazoezi, tafakuri, n.k.).
Ndio miaka mingapi sasa? (naambiwa swali hili sio vizuri kuuliza wanawake!)
Mija ilikopigwa picha ya mzaa chema kuna uhusiano wowote na Kyela ama Kigoma hivi?
Asanteni woote kwa pongezi, naona zote zimenijia mimi na si mama. Hata mimi binafsi ninaamini siku hii ni ya mzaliwa sio mzaaji, maana kama ingekuwa hivyo basi baba yeye haki yake iko wapi? Mwandani umesema kweli juu ya hilo kwa upande wa baba.
Mwaipopo,
Hii picha sina hakika sana imepigwa wapi lakini kwa asilimia 99.8 ninaamini ni Mitaa ya Shinyanga au Mwanza.
Ndesanjo,
Kweli kabisa si vizuri kumuuliza mwanamke umri wake (sijui hata ni kwa nini) lakini mimi kiumri nimekuzidi mwaka mmoja haya piga mahesabu sasa hapo.
Hebu acha utani, umenizidi mwaka mmoja? Yaani ina maana hutakuwa ukinipa shikamoo. Hebu toka kule, acha utani.
Post a Comment
<< Home