27 February 2013

Ayaan Hirsi Ali..

Posti yangu iliyopita niliuliza swali la kumtambua mdada kwenye picha, wengi mmepatia, ni dada Ayaan Hirsi Ali, mwanasiasa msomali aliyeamua kuipinga dini yake. Kwa habari zaidi msikilize...

....lakini kwa ufupi bado sijaielewa vizuri akili yake, sijui wenzagu mnasemaje?



2 Comments:

At Thursday 28 February 2013 at 08:06:00 GMT, Blogger emuthree said...

Kila mtu atauchukua/ataubeba mzigo wake mwenyewe, SIKU HIYO IKIFIKA!

 
At Thursday 28 February 2013 at 16:52:00 GMT, Anonymous Anonymous said...

Mayowane na wadau wengine,

Hiki kichwa matata sana lakini pale alipotia chumvi mchakato wa makaratasi ndipo alipoharibu.

Tukirudi kwenye analozungumza hakuna cha ajabu watu wamequestion Biblia na Koran tangu mwanzo hadi leo. Lakini wengi wa walioquestion ua wanaoquestion mafundisho ya Biblia na Koran wamekuwa ni wanaume. Ukitaka kuona jinsi gani watu wanavyoquestion mafundisho ya Biblia na Koran ni jinsi dini hizi mbili zilivyo na madhehebu mengi yenye kupingana katika mafundisho yake.

Kama unakumbuka somo la Isimu la Mwalimu Kachepa kule Chuo cha Sanaa, Bagamoyo kwa kumsikiliza anachongea, uchaguzi wa misamiati anayotumia na mada na hoja anayoitoa utaweza kuapata picha fulani ya akili ya huyu mdada.

Hapa ingependeza sana kama tungepata mdahalo kati ya huyu dada na walimu wa dini ya Kiislamu. Mdahalo ulalie kwenye nguvu ya hoja siyo hoja za nguvu ingekuwa bonge la mdahalo. Au mnasemaje?

Nene Guku!

 

Post a Comment

<< Home