29 February 2012
Njia 4 za malezi.... Ni njia gani unayoitumia?
Hii ni tafsiri ya mada iliyopita ya njia 4 za ulezi ambapo msomaji wangu mmoja aliomba niiandike kwa kiswahili... Video hapo huu ni kibwagizo tu. Karibuni tena!
Ulezi wa kimabavu(Authoritarian Parenting)
Hii ni aina ya ulezi ambapo wazazi huweka sheria kali kwa watoto wao ambazo ni lazima wazifuate wapende au wasipende. Kushindwa kufuata sheria hizo hupelekea kupewa adhabu. Wazazi hawa huangalia zaidi watoto kuwa na utii na hadhi kwa watu zaidi ya kuwa huru. Ni ulezi ambao wazazi wenyewe mara nyingi huwa hawana sababu maalumu ya kuweka sheria wanazoziweka na pale wanapoulizwa huishia kusema "unatakiwa ufanye kwa sababu nimesema hivyo". Watoto wanaolelewa kwa njia hii mara nyingi huwa na nidhamu sana ila ni ya woga.
Ulezi wa Kimamlaka(Authoritative Parenting)
Hii ni aina ya ulezi ambao mzazi huwa na mamlaka kwa kwa watoto lakini si kwa mabavu. Mzazi hutengeneza sheria na mwongozo mzima kwa watoto na huweka wazi sababu ya sheria zile. Huwa tayari kuongea na watoto na kuwasikiliza hoja zao. Watoto hawa wanapokosea mara nyingi hupewa msamaha zaidi ya adhabu. Wazazi hawa hulenga zaidi watoto wao kuwa na uthubutu katika jamii.
Ulezi wa Uhuru(Permissive Parenting)
Hii ni aina ya ulezi ambao kwa jina lingine huitwa ulezi wa kudekeza. Wazazi wa aina hii mara nyingi hupenda kuwaacha watoto huru wafanye kile watakacho, hawaweki sheria zozote za kuwaongoza watoto, huwafanya watoto kama marafiki zao zaidi ya uzazi na hata watoto wanapokosea huwa hawapewi adhabu yoyote ya kurekebisha tabia na badala yake hutetewa.
Ulezi wa kutojihusisha(Uninvolved Parenting)
Kwa jina lingine huitwa ulezi wa kutelekeza, Ni ulezi ambao mzazi hajihusishi na maendeleo ya mtoto wala hana malengo yoyote ya mbeleni ya mtoto huyo. Haangalii kama mtoto yupo au hayupo, alienda shule au hakwenda, alikula au hakula, wazazi hawa wanachojua ni kuzaa na kusahau na mara nyingine huwakataa hata watoto wao.
Je ni njia gani unayoitumia?
| Reactions: |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
nimelelewa ki mamlaka kwakweli
NIMELELEWA HOVYO, AINI MIMI NITALEA MALEZI YA UHURU NA MAMLAKA. NACHANGANYA VYOTE HAPA
tumefundishwa kushukuru kwa kilajambo, mimi ni yule anonymous niloomba utafsiri mada hii na kwa moyo wa dhati kabisa ninarudi hapa kutoa shukrani zangu za dhati.
Kwa kweli mada hii itatusaidia wengi kujitambua kua tupo/tunalea watoto wetu ktk malezi yapi. Nimeielewa vizurisana hii mada.
kwa mara nyingine tena nakushukurusana da Mija na Mungu akubariki na akupe nguvu na afya tele uendelee kutuelimisha, kweli Ulizaliwa Uwe Mwanamke wa Shoka haswaaaa!!!! Thanx
Mmmmmh!Najifunza tu hapa! Najua kulea watu wazima lakini!:-(
Nakubaliana na Kamala. Hakuna jina moja inayofaa. Inabidi kuchanganya zote kila moja kwa wakati wake unaofaa!
Post a Comment