29 June 2011

Mzee Ambrose Shija Sayi... Leo umetimiza miaka 22 kamili tangu ulipotutoka..!!


Mzee Sayi pichani, baba mzazi wa Grace, Sabina, Antimi, Mija, Nyanzu na Nyanzala. Leo umetimiza miaka 22 tangu ulipotutoka mwaka 1989. Tunamshukuru sana Mungu kwa kutupa baba kama wewe ambaye ulitupenda na kutujali kwa moyo wako wote, kwa kweli katika watu ambao wanaweza kuringa kwamba walipata baba safi, sisi ni wamoja wapo. Lakini kwa mapenzi ya Mungu aliona akuchukue ili nasi tuweze kufika ambako ametupangia tufike.

Basi baba kwa taarifa yako huku ulikotuacha sisi tunaendelea vizuri sana na maisha, labda tukupe tu habari nzuri ambayo unapaswa kuijua, kwamba ulipoondoka uliacha mjukuu mmoja lakini sasa unao 12 na kitukuu kimoja 1.. hawa ni
Happy, Shija, Andrea, Adrian, Anais, Alexanda, Alicia, Mija, Manjula, Elizabeth, Asiimwe na Mukama. Kitukuu ni Richard.

Baba tunatumaini kwa habari hii sasa hivi unafuraha vibaya sana kwani kizazi chako kinaendelea...

Basi tunaomba Mungu azidi kuwa nawe uko uliko ambako kila mtu hana budi kuwako.
Amen.

BASATA: NGOMA ZA ASILI HAZIJATOWEKA


Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (Kulia) akisisitiza jambo juu ya ngoma za asili wakati akizungumza na wadau wa sanaa kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Jivunie Tanzania,Bi.Mariam Ismail na Agnes Kimwaga,Afisa Uhusiano wa BASATA.


Mdau kutoka Business Times,Humphrey Shayo akitaka kujua juu ya sanaa mbalimbali za asili zinazofanywa na kundi la la Sanaa la Jivunie Tanzania na nafasi yake kwa sasa.


Baadhi ya wasanii wazee wa Kundi la Sanaa la Jivunie Tanzania wakicheza Ngoma ya Manyanga na kutambika kabla ya wasanii wengine wa kundi hilo hawajaja Jukwaani kumwaga burudani kedekede za asili.


Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema kwamba,ngoma za asili bado zina hadhi na nafasi kubwa katika jamii zetu ingawa kwa maeneo ya mijini mwamko wa sanaa hiyo unaonekana kupungua tofauti na zamani.
Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba,ngoma za asili zipo kama kawaida na zimekuwa na nafasi kubwa mikoani ambako zimekuwa zikivuta watu wengi.
“Kuna matamasha makubwa ya ngoma za asili kama yale ya Makuya, ya kale yanapokutana na ya sasa, Bujora na Chamwino.Matamasha haya yamekuwa yakivuta watu wengi sana hivyo,dhana kwamba ngoma za asili zimetoweka si sahihi” alisema Materego.
Aliongeza kwamba,kinachotokea kwa sasa ni athari za utandawazi kwenye ngoma za asili ambazo zimebadili upepo wa sanaa hiyo maeneo ya mijini lakini akasisitiza kwamba,bado hata maeneo ya mijini kuna vikundi vingi vya ngoma za asili vinavyofanya vizuri.
“Utandawazi kwa kiasi fulani umeathiri ngoma za asili hasa maeneo ya mijini lakini bado hata hivyo kuna vikundi vingi Baraza limevisajili na kuvisimamia mijini kama hiki kilichotuburudisha leo cha Jivunie Tanzania” Alisisitiza Materego.
Alitoa wito kwa wakuzaji sanaa kujikita kwenye kuandaa matamasha mbalimbali ya sanaa za asili ili kuzidi kuisambaza sanaa hiyo ambayo ni muhimu sana kwa utambulisho wa utamaduni wetu na kwa muda mrefu imelijengea heshima taifa letu.
“Ni kweli tuna matamasha mengi ya ngoma za asili lakini ni wazi juhudi nyingi zinahitajika ili kujenga mwamko zaidi katika sanaa hizi.Ni muhumu ikaeleweka kwamba,sanaa hizi zinabeba kila kitu ndani ya jamii” alimalizia Materego.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Jivunie Tanzania,Bi.Mariam Ismail alisema kwamba, watanzania wasiache kupenda ngoma za asili na kupapatikia vitu vya nje kwani kufanya hivyo ni kupuuza malezi na historia za jamii zao.
Jukwaa la Sanaa kila mwisho wa mwezi linapambwa na burudani mbalimbali na kwa mwezi huu Kundi la Sanaa la Jivunie Tanzania kutoka Temeke Dar es Salaam lilitoa burudani kedekede za asili.

19 June 2011

Fredrick Chiluba hatunaye tena..Rais wa zamani wa Zambia bwana Fredrick Chiluba amefariki dunia jana tarehe 18-06-2011. Kwa habari zaidi fungua hapa.

16 June 2011

Labda Big Brother ihamie Ikulu... Hoja safi kutoka kwa Kitururu!!

...Hivi Big Brother si tuihamishie IKULU ili tuone kila kitu kinachofanyika katika maamuzi yatufanyao wenye nchi iliyo tajiri watu wake wawe dunia nzima wanasifika kwa umaskini?


Mie MKINIPA URAHISI,..
..samahani Urais,....
.... haki ya nani nisinge futa BIg Brother ila ningeihamishia kila ofisi za serikali ili wananchi waone wanavyo fanywa vibaya na watu hata kuguna kama tamu hawaguni vizuri!:-(

11 June 2011

Hongera Manjula kwa kutimiza miaka 3..!! 10/06/2011

Manjula na rafiki yake mpenzi Hello Kitty

Manjula katika pozi la siku..!!

Furaha tele..!!

Hapa anapuliza mshumaa kuiambia jamii kwamba mwaka wa tatu ndo huo moto wowote utakaokuja mimi nitauzima tu..!!

Manjula akikata keki yake...

Kazi ya mkono wa Mama Manjula a.k.a Da' Mija.

Kaka Isaack akiwa mbaaali kimawazo... je mdau unaweza kudhani alikuwa akiwaza nini hapo??

Familia yetu ina wanaume wachache jamani, ni Isaack na Mukama tu..!!

Mwisho wa shughuli Manjula anang'ng'ania kulala na kibanio cha nywele na kadi yake...utoto!!


Mwanzoni alijulikana sana kwa jina la Baby Manjula, lakini siku hizi ukimwita hiyo anakwambia I'm not baby,..I'm toddler, upo hapo mdau? Siku zinakwenda Manjula wa juzi tu sasa amefikisha miaka mitatu na ameshaanza kuwa na uwezo wa kukukosoa unapokosea jambo au unapotaka kumpelekapeleka bila mpangilio wowote.

Kwa kweli ninamshukuru sana Mungu kwa mtoto huyu, Manjula ana afya nzuri, ana akili timamu na anatabia zoooote za kitoto na za kibinadamu kiujumla, analia panapotakiwa na hata pasipotakiwa kulia, anacheka panapotakiwa na hata pasipotakiwa kulia, anang'ang'ania vitu vyake na hata visivyo vyake, siku aking'ang'ania kubwebwa kang'an'gania na mengine meeeengi, kwa yote haya namshukuru Mungu kwani ndio furaha ya mzazi kwa vile huonyesha kwamba mtoto wake ni timamu.

Happy Birthday Manjula!!

09 June 2011

Msaada tutani.. Renatha Benedikto unatafutwa!!

Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu. Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/namtafuta-renatha-benedicto.html)

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio. Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.
Email yangu ni changamoto@gmail.com