Nchi za kiafrika ni ngumu kujua nani ni tajiri kwa sababu zifuatazo
1. Watu wanakwepa kodi hivyo serikali ni ngumu kujua pato halisi la kila mwananchi
2. Kukithiri kwa rushwa hivyo kufanya pesa nyingi kufichwa
Kwa Misingi hiyo basi, Serikali inawajua Matajiri wasafi tu na wenye kulipa kodi na hali halisi ya uchumi ni kwamba haiwezekani kuwakadiria kwa hakika,
Katika Tanzania, Tajiri hatajulikana mpaka matatizo hayo yatakapotatuliwa
Jana niliomba msaada wa swali lililokuwa likinitatiza kujua jibu lake. Nashukuru mdau mmoja ametoa jibu (hilo hapo juu) ambalo nimekubaliana nalo kwa asilimia zote, wadau kutokana na jibu lake nimepata swali lingine, HIVI NI KWA NINI NCHI ZA KIAFRIKA ZINASHINDWA KUWEKA KIKAKATI IMARA YA KUHAKIKISHA KODI INALIPWA NA KILA ANAYEHITAJIKA KULIPA? NA NI KWANINI RUSHWA HAITHIBITIWI AFRIKA? NANI WA KULAUMIWA HAPA, WANANCHI AU VIONGOZI? Natanguliza shukrani wadau.
16 July 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

3 comments:
wa mtazamo wangu nadhani ni viongozi ndio wa kulaumiwa. Pia nazani kama serikali ingekataa kupokea rushwa basi kusingekuwa na rushwa.
Sa Mija,
Mie nafuatilia swala hili la maendeleo kimasomo na kwa ujumla kuna sababu nyingi zinazoingiliana.Lakini sababu kubwa kuliko zote ni "poor institutions". Lakini tuko pampja kutafuta ukweli kwani kuana blogu letu la maoni ya wachumi tulionanzisha (http://wachumi.blogspot.com/),nia na kusudi ilikua kuendeleza conversation kama hizi.Kwahiyo hongera!Sante MM
Wakati tunajadili tukumbuke tu ni wananchi ambao hugeuka viongozi.
Kwa hiyo tuangalie wananchi hujifunza nini ambacho wakigeuka viongozi husahau?
Ni hilo tu!:-(
Post a Comment