13 July 2007

Nyapara na Manamba.. waraka toka kwa Tungaraza MtiMkubwa.

Siku moja nilipata kuangalia filamu ya maisha ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Marehemu Kapteni Jean Baptist Bokassa. Baada ya kuitazama ile filamu nikashikwa na tafakuri juu ya tabia za binadamu hususani pale wanapokuwa na madaraka.

Jambo moja nililolibaini katika tafakuri yangu ni kwamba wanaadamu wengi wanapenda madaraka. Zaidi ya hivyo madaraka yanaweza kulevya vibaya kuliko pombe kali au bangi. Watu hupata madaraka ama kwa kuzaliwa kwenye koo iliyopo madarakani mathalani wafalme, malkia, masultani na watemi, au kwa taaluma, au kwa kuteuliwa, au kupigiwa kura, au kwa kujipachika, au kwa kunyang'anya, au kwa mizengwe.

Ili kujikweza kimadaraka watu hunakshi nomino zao na badala ya kuitwa majina yao huwa wanaitwa Mtukufu Rais, Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Spika, Waziri, Naibu, Katibu, Mkuu, Mzee, Baba wa Taifa, Ofisa, Dokta, Profesa, Mtakatifu, Mchungaji, Askofu, Muinjilisti, Kateksiti, Maalim, Alhaji, Shehe, Imam, Walii, Maulana, Ayatollah, Chifu, CEO, Mheshimiwa Balozi, Jenero, Afande, Kamanda, Mtaalam, Bwana, Bibi, na kadhalika.

Madaraka humpa mtu uwezo wa kuelekeza muelekeo wa tabia za wale anaowaongoza hali kadhalika mfumo, utaratibu, na muundo wa taasisi anayoiongoza. Madaraka yanaweza kujenga, kubomoa, au kuharibu tabia ya mtu au taasisi. Mifano ya taasisi na watu waliojengwa, kubomolewa au kuhitilafiwa tabia kwa sababu ya madaraka ni mingi sana. Pia madaraka huweza kutukuza au kudhalilisha. Wapo watu kwa sababu ya umakini wao katika madaraka nomino zao zilinakshiwa Utakatifu na wale waliopotosha madaraka yao walinakshiwa Udikiteta au Fashisti.

Madaraka hujenga tabaka la viongozi na maamuma. Mfano wa haya makundi ya viongozi na maamuma ni kama yale wahubiri na waumini, wanasiasa na wananchi, viongozi na wafanyakazi, afande na kuruta, na kadhalika. Kuna wakati utawasikia wale walio madarakani wakisema "..Watu wangu wako wapi?.." "..Vijana wangu wanahitaji..." ...Watu wangu tuliwaahidi kuwajengea zahanati.." na kadhalika.

Wiki kadhaa zilizopita niliandika kuhusu muelekeo wa Mheshimiwa Spika na Naibu wake na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Tanzania la sasa. Ukifuatilia utaratibu wa hoja, maswali, na majibu bungeni hutasita kukubaliwa kuwa bunge letu limekuwa kama la Nyapara na Manamba. Mfano mmoja huo hapo chini:


Spika azuia maswali ya afya magerezani

Basil Msongo, Dodoma
HabariLeo; Thursday,July 12, 2007 @00:04
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta jana alizua gumzo bungeni baada ya kuzuia Wizara ya Mambo ya Ndani isijibu maswali matatu ya nyongeza kuhusu hali ya afya magerezani ikiwamo Ukimwi na magonjwa mengine ya kuambukiza.

Alitoa uamuzi huo wakati Naibu Waziri, Lawrance Masha akijiandaa kuyajibu baada ya kujibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Ruhwanya (CHADEMA) aliyetaka kujua ni hatua gani zinachukuliwa kuhakikisha Ukimwi hausambai magerezani hasa kwa watoto waliochanganywa na watu wazima kutokana na uhaba wa jela za watoto.

Kabla ya Spika Sitta kuzuia majibu ya nyongeza, Masha alisema si kweli kuwa wafungwa wanaandamwa na maradhi ya kuambukiza magerezani ukiwamo Ukimwi. Akiuliza swali la nyongeza, Mhonga alimuuliza Naibu Waziri endapo atakuwa tayari kubadili kauli hiyo endapo mbunge huyo atampatia ushahidi kuthibitisha kukithiri kwa magonjwa ya kuambukiza magerezani ukiwamo Ukimwi.

Mbunge huyo pia aliuliza ni bajeti kiasi gani imetengwa kukabiliana na Ukimwi magerezani. Hapo Spika akaamuru swali hilo lisijibiwe. Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa (Chadema) alisema, taarifa ya Tume ya Jaji Kissanga ilibainisha kuwapo kwa tatizo hilo katika magereza takriban yote nchini hivyo akaitaka wizara hiyo ieleze endapo taarifa ya tume hiyo si sahihi.

Spika aliamuru pia swali hilo lisijibiwe hali iliyozua gumzo miongoni mwa wabunge hasa wa kambi ya upinzani. Kabla ya uamuzi wa Spika, Masha aliliambia Bunge kuwa serikali imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kuwa Ukimwi hausambai magerezani ikiwa ni pamoja na kuzuia aina yoyote ya ngono magerezani na kuwatenga wafungwa na mahabusu wanawake na wanaume.

Kwa mujibu wa Masha, watoto wanatengwa na watu wazima magerezani ingawa Mbunge Mhonga alisema kuna jela tatu tu za watoto nchini, na moja ya vijana. Alisema viwango vya maradhi magerezani si tofauti na katika jamii kwa kuwa katika kila gereza kuna huduma ya tiba kwa ajili ya wafungwa.

Ili kudhibiti magonjwa ya kuambukiza magerezani, askari kusimamia kazi ya kuwanyoa wafungwa na kutaja vifaa vinavyotumika kuwa ni mikasi, nyembe, brashi, mafuta maalumu ya kunyolea na sabuni.

32 comments:

 1. Spika amuokoa Karamagi
  Akiri mjadala ulikuwa mkali
  NA WAANDISHI WETU, DODOMA
  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta jana alilazimika kukiuka baadhi ya kanuni kumuwezesha Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kujibu hoja wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha makadirio ya matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2007/08.
  Hatua hiyo ilifuatia kundi la wabunge kusimama kwa wakati mmoja, baada ya kifungu cha kwanza kinachohusu mshahara wa waziri katika bajeti hiyo kusomwa.
  Hata kabla Spika Sitta hajamaliza kuhoji kwa kusema ‘kifungu hicho kinaafikiwa’, wabunge zaidi ya 15 walisimama kutaka kutoa hoja mbalimbali.
  Kuona hivyo, Spika alianza kuwaorodhesha na baadaye kumwita mmoja baada ya mwingine, lakini katika kuokoa muda, alibadili utaratibu na kutaka wale wenye hoja kuhusu umeme vijijini wavitaje vijiji wanavyotaka vipatiwe umeme.
  Kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele, aliona kuwa kila mbunge kutaja vijiji vyake kungeweza kuchukua muda zaidi.
  Hivyo alitumia rungu lake kuruhusu kukiukwa kwa kanuni inayowalazimu wabunge kunukuu miongozo mbalimbali kabla ya kutoa hoja kuhusu kifungu kinachotaka kupitishwa.
  Baada ya hatua hiyo, baadhi ya wabunge waliwasilisha hoja zao nyingi zikihusu usambazaji wa umeme vijijini, ulipwaji wa fidia kwa wananchi ambao mazao yao yalikatwa kwa ajili ya kusambaza umeme, pamoja na suala la madini.
  Muda wote wakati hoja zikiwasilishwa, Spika Sitta alikuwa akiingilia kati kuhakikisha mjadala unakamilishwa ndani ya muda uliopangwa.
  Alimuelekeza Waziri Karamagi kutoa ahadi kwamba hoja zote za wabunge kuhusu umeme vijijini azijibu kwa maandishi, naye aliafiki.
  Kabla ya kumruhusu Waziri Karamagi kuhitimisha, Sitta alikiri kwamba, mjadala ulikuwa mkali katika kamati ya matumizi na kwa kuwa zilibaki dakika chache kufikia muda wa kuahirishwa Bunge, wa saa 1.45 usiku, hotuba hiyo ya makadirio ya matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2007/08 ulipitishwa kwa uamuzi wa jumla kwa mujibu wa kanuni za Bunge.
  Baada ya hotuba hiyo kupitishwa, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Kabwe Zitto, aliwasilisha ombi la kuwasilisha bungeni hoja binafsi inayotaka kuundwa kwa kamati kuchunguza ukweli kuhusu mkataba mpya wa madini uliotiwa saini na wizara hiyo.
  Alisema ufafanuzi wa Waziri Karamagi kuhusu suala hilo unapingana na agizo la Rais Jakaya Kikwete linalotaka mikataba ya zamani ya madini ipitiwe kwanza kabla ya kuingia mipya.
  Spika Sitta alimjibu kwamba, hiyo ilikuwa taarifa na haikuwa na madhara, na kwamba itafanyiwa kazi baada ya kuwasilishwa rasmi kwa maandishi.
  BAADHI ya wabunge wamemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kwenda kwenye majimbo yao kuwaeleza wananchi chanzo cha kuchelewa kupata umeme.
  Wabunge hao walitoa ‘mialiko’ hiyo jana walipokuwa wakichangia hotuba ya waziri huyo kuhusu makadirio ya matumizi ya wizara kwa mwaka wa fedha 2007/08.
  Walimtaka Waziri Karamagi au Naibu wake, William Ngeleja kutembelea majimboni mwao na kuwaeleza wananchi chanzo cha kuchelewa kupata umeme.
  Bujiku Sakila (Kwimba- CCM) alisema kwa zaidi ya miaka 11 anafuatilia umeme bila mafanikio, na kumuomba Karamagi kufanya ziara Kwimba kuwaeleza wapiga kura kulikoni.
  Alisema maeneo ya Igula, Hungumalwa na Mwamashimba hayana umeme na kwa miaka yote amekuwa akipewa ahadi ambazo hazijatekelezwa.
  Sakila alisema maeneo hayo yana zaidi ya shule saba za sekondari, zahanati na viwanda viwili vya kuchambua pamba ambavyo ni muhimu kwa uchumi wa wakazi wa maeneo hayo, lakini hakuna umeme.
  “Hivi sasa naogopa kusimama kwa wananchi, kwani nimeshatoa ahadi nyingi ambazo nilikuwa napewa wizarani. Namuomba waziri atembelee maeneo hayo, tena usiku ili ajionee hali ilivyo,” alisema Sakila.
  Naye Jenista Mhagama (Peramiho- CCM) alimtaka Ngeleja kwenda jimboni kwake na kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu umeme.
  “Nimekwisha kuzungumza sana, ni vyema tukaenda na waziri ili akajieleze kwa wananchi kuhusu umeme,” alisema.
  Aliishauri serikali kuwa na mipango endelevu ili kuwaondolea umasikini wananchi wa vijijini kwa kuwapelekea umeme.
  Kwa upande wake, Kaika Telele (Ngorongoro-CCM) alisema wilaya za wafugaji zina utajiri mkubwa, lakini miundombinu yake ni mibovu, hivyo ni vyema waziri akatembelea na kujionea hali ilivyo.
  Alisema alielezwa kuwa Wilaya ya Ngorongoro inaweza kupata umeme ifikapo mwaka 2015, ahadi ambayo inapingana na falsafa ya Rais Jakaya Kikwete ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya.
  Aliiomba serikali kuipa Ngorongoro upendeleo maalumu ili ipate umeme, kwani imeahidiwa kwa muda mrefu, ahadi ambayo haijatekelezwa. Aliomba wasaidiwe jenereta wakati wakisubiri umeme.
  Wakati huo huo, Kabwe Zitto (Kigoma Kaskazini- CHADEMA), ametoa shutuma nzito dhidi ya wizara hiyo kuwa imeingia mkataba mpya na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick, hivyo kukiuka maagizo ya Rais Kikwete.
  Alidai wizara imeingia mkataba mpya wakati timu iliyoteuliwa kupitia upya mikataba ya zamani haijakamilisha kazi yake.
  Zitto alidai Waziri Karamagi hivi karibuni alitia saini mkataba mpya na Kampuni ya Barrick jijini London, Uingereza. Alidai kutiwa saini kwa mkataba huo nje ya nchi kunaashiria kuwepo kwa vitendo vya rushwa.
  Alitahadharisha kuwa muda mfupi unaokuja Barrick inaweza kuwa kampuni pekee inayomiliki migodi mikubwa nchini, hivyo kuweza kurudisha nyuma harakati za kukuza uchumi. Alidai hivi sasa inamiliki migodi minne ya dhahabu.

  ReplyDelete
 2. Karamagi una ahadi nyingi hewa -Wabunge

  2007-07-17 11:06:02
  Na Mary Edward, PST Dodoma


  Waziri?wa Nishati na Madini, Bw. Nazir?Karamagi, jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya wabunge kumtaka aeleze sababu za kutoa ahadi hewa zisizotekelezeka, ikiwemo marekebisho ya mikataba ya madini, usambazaji umeme na matumizi ya gesi asilia.

  Zaidi ya wabunge 12 waliochangia mjadala huo jana walimtaka Bw. Karamagi kutoa maelezo ya kina kuhusu sababu za wachimbani wa madini kutoka nje kuhodhi maeneo makubwa na kufanya utafiti muda mrefu, huku wengine wakiongezewa muda, huku wazalendo wanaojulikana kama wachimbaji? wadogo wakitengewa maeneo finyu na kuhamishwa bila kulipwa fidia mara `wakubwa` wanapogundua madini.

  Mbunge wa Viti Maalumu, Dora Mushi (CCM), alimtaka Waziri Karamagi kulieleza Bunge hatua iliyofikiwa na Wizara yake katika makubaliano ya madini ya Tanzania kupitia mkondo mmoja, ili kuleta manufaa kwa Taifa na kuzuia mataifa jirani kutumia madini ya Tanzania kujitangaza na kujichotea mabilioni huku nchi ikizidi kugubikwa na umaskini.

  Bi. Mushi alisema kwamba, badala ya wageni kuja Tanzania kununua madini ya Tanzanite wanakwenda Afrika ya Kusini, ajmabo ambalo alisema halimuingii akili na kumtaka waziri kutoa maelezo.

  Mbunge wa Rufiji, Bw. Idrisa Mtulia (CCM), aliishauri Serikali kuliwezesha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kusimamia usafirishaji wa madini kwenda nje, na kuhakikisha kwamba rasilimali hiyo haitumiwi vibaya na nchi jirani.

  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), alimtaka Bw. Karamagi kulieleza Bunge sababu zilizomfanya asaini mkataba mpya wa uchimbaji madini na Kampuni ya Barrick nje ya Nchi, wakati serikali ikiendelea kuipitia upya mikataba ya madini.

  Zitto alisema kuwa, Bw. Karamagi alisaini Mkataba huo nchini Uingereza na kwamba kampuni hiyo itachimba madini katika eneo la Buswagi na kudai kuwa, kitendo hicho kina sura ya rushwa.

  ``Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni zake aliahidi kupitia mikataba yote ya madini, lakini cha kushangaza leo Serikali hiyo hiyo tena imesaini mkataba mpya na Kampuni ya Barrick tena nje ya nchi, wakati Watanzania hawajui nini kinachoendelea.

  Kadhalika alihoji sababu ya kuondolewa kwa kipengele cha asilimia 15 ya kodi kwa wachimbaji bila kufikishwa bungeni, jambo alilodai ni watendaji wa Serikali kuingilia madaraka ya Bunge hivyo kuitaka Serikali kutoa maelezo ya suala hilo na endapo kama itabainika ni kweli watendaji hao walihusika, iundwe kamati na waitwe kuhojiwa.

  Bw. Zitto hakuishia hapo, aliendelea kuhoji uhalali wa Serikali kuuza asilimia 55 ya hisa zake katika Kampuni ya Bulyanhulu kwa bei ya kutupwa na sasa kutaka kununua tena hisa.

  ``Tunafahamu kuwa serikali ilikuwa inamiliki asilimia 55 ya hisa katika kampuni ya Bulyanhulu na baadaye kuiuza kwa bei ndogo ambayo ni shilingi bilioni 5, wakati thamani ya hisa hizo ilikuwa trilioni 1.1, sasa kwa nini iliamua kuuza hisa hizo na kwa nini tena leo inataka kununua hisa?`` Alihoji Zitto.

  Naye Mbunge wa Lupa, Bw. Victor Mwambalaswa, (CCM) aliitaka Serikali kushughulikia haraka marekebisho ya Sheria mpya ya madini kwa maelezo kuwa iliyopo sasa inatoa mwanya kwa wawekezaji wa nje kubadili majina na kuendelea na kazi kwa jina lingine bila faida yoyote kwa Tanzania.

  Kwa upande wake Bi. Josephine Genzabuke (CCM), Viti Maalum alimtaka Bw. Karamagi kulieleza Bunge ni lini atawasilisha sheria ya kuruhusu mashirika mengine kuruhusiwa kuzalisha na kusambaza umeme kwa wananchi moja kwa moja hususan maeneo ambayo hayajafikiwa na TANESCO.

  Naye Mbunge wa Bukene, Bi. Teddy Kasella-Bantu, aliitaka Serikali kubadili mfumo wa magari yote kutumia mafuta badala yake yatumie gesi na kwamba kwa kufanya hivyo kutaipunguzia gharama kubwa za matumizi kwa kuwa gharama ya gesi ni nafuu zaidi ikilinganishwa na mafuta.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Nzega, Bw. Lucas Selelii (CCM), alimtaka Bw. Karamagi kueleza sababu za ahadi hewa za kupeleka umeme jimboni kwake bila utekelezaji na kwamba wataelewana vibaya na Waziri huyo, hivyo njia pekee ni kutoa maelezo ya lini umeme utepelekwa jimboni kwake kutimiza ahadi ya Serikali.

  Naye Mbunge wa Viti Maalum, Bi. Mhonga Ruhwanya, aliimtaka Bw. Karamagi kueleza Bunge ni lini Mkoa wa Kigoma utapatiwa umeme kwa kuzingatia ahadi ya Rais Kikwete, aliyoitoa wakati alipotembelea mkoa huo na kupokelewa na vibatari ambapo aliahidi kuwa mkoa huo utapatiwa umeme, lakini hakuna kinachoendelea hadi sasa.Bunge lilipokaa kama kati jana jioni ili kupitisha bajeti hiyo, wabunge karibu 10 walisimama ili kushikilia mashahara wa waziri, kuonyesha kuwa walitaka maelezo zaidi kutokana na ahadi nyingi hewa.

  Mbunge wa Gando (CUF), Bw. Khalifa Suleiman Khalifa, alilazimika kumkumbusha Spika utaratibu kwamba hali kama hiyo ikitokea, analazimika kurejea kwenye kiti cha Spika na kuendesha mjadala tena kuhusu wizara husika ili hoja za wabunge zijibiwe vyema.

  Spika alikubaliana na ombi hilo, akaondoka kwenye kiti cha umwenyekiti wa kamati na kukalia uspika. Lakini alipouliza ni wangapi wanataka mjadala uendelee, karibu wabunge wote wa upinzani walisema ``ndio``, lakini wale wa CCM ambao ni wengi walisema ``siyo``, na hivyo Mheshimiwa Karamagi akapumua, bajeti yake ikapita.

  SOURCE: Nipashe

  ReplyDelete
 3. Tupia jicho kwenye blog hii changa
  kama unatakusapot weka kwenye link
  yako Kila mwanzo kuna ugumu wake
  www.kennedytz.blogspot.com
  au kennytz

  ReplyDelete
 4. Unyampara nilifikiri kuwa Nyerere aliukataza.Duh!Hili bunge ambalo Waziri Mkuu anaweza kumkataza Spika wa bunge katika maswala ya bunge , mimi naliogopa.Lakini wana mishahara mizuri, kama mtu kaenda bungeni kula!

  ReplyDelete
 5. NYAMPARA KUWABURUZA MANAMBA KUPIMA UKIMWI

  Wabunge kupimwa ukimwi Jumamosi

  na Rachel Chizoza, Dodoma


  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, jana alitangaza kuwa siku ya Jumamosi itakuwa ni maalumu kwa wabunge wote kupima afya zao kujua kama wameambukizwa virusi vinavyosababisha ukimwi au la.

  Akizungumza mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni jana, Sitta alisema kuwa, upimaji huo ni sehemu ya mwitikio wa kampeni ya kitaifa inayomtaka kila Mtanzania kupima ili kujua hali yake kiafya.

  Akitoa tangazo hilo, Sitta alisema kuwa yeye mwenyewe atakuwa wa kwanza kupima, hivyo hakuna mbunge yeyote atakayekuwa na sababu ya kutofika siku hiyo na kupima afya yake.

  Alisema zoezi hilo la upimaji litaanza majira ya saa 3:00 asubuhi baada ya kumalizika kwa mbio za wabunge za kilomita tano zitakazoanzia kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa na kuishia katika viwanja vya Bunge.

  “Ili nihakikishe wabunge wote mnapima mimi nitaongoza zoezi hilo la kupima kwa kuwa mpimaji wa kwanza,” alisema Spika.

  Alibainisha kuwa zoezi la upimaji linapaswa kuwa la wazi na litafanyika mbele ya watu kama alivyofanya Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo, Jumamosi iliyopita.

  Alisema uwazi huo utasaidia pia wananchi kuona mfano utakaoonyeshwa na wawakilishi wao.

  Wakati huo huo wakazi wa mji wa Dodoma wameonyesha kuhamasika kupima afya zao baada ya kuona Rais Kikwete akijitokeza kupima hadharani.

  “Tumehamasika sana na naamini wananchi wengi watajitokeza kupima, maana kitendo cha Rais kupima hadharani kinatia moyo,” alisema.

  Walisema awali walikuwa wakiogopa kupima kwa kujua kwamba mtu akikutwa na virusi vya ukimwi atakufa mapema kutokana na unyanyapaa uliokuwepo katika jamii.

  Walisema hivi sasa jamii imeelimishwa kwa kiasi kikubwa kuhusu kuondoa unyanyapaa kwa waathirika na umuhimu wa kupima ili kujua afya zao.

  Walisema utoaji wa dawa za ARV’s pia umeongeza kasi ya kupima kwani wananchi wameelewa kwamba, wakikutwa na maambukizi hautakuwa mwisho wao wa kuishi kutokana na kuwepo kwa dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa ukimwi.

  Waliitaka serikali kutoa adhabu kali kwa watumishi wa sekta ya afya ambao hawawezi kutunza siri za wagonjwa na watu wanaokwenda kupima kwani wao ni kichocheo cha kuwafanya wananchi waogope kujitokeza kwenda kupima afya zao.

  Wakazi hao wa mjini Dodoma walisema ni vema zoezi hilo la upimaji wa afya liendeshwe pia katika maeneo ya vijijini kwani wagonjwa hawapo mijini pekee, maana kutowapima wananchi wa vijijini ni kurudisha nyuma vita dhidi ya ukimwi.

  ReplyDelete
 6. Sitta awatoa hofu wabunge kesho

  2007-07-20 10:45:12
  Na Dustan Bahai, Dodoma

  Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta amewatoa hofu wabunge baada ya jana kuwaona wamenyong`onyea alipowataka kujitokeza kupima Ukimwi, kesho.

  ``Mbona wabunge leo mnaonekana mmepooza au ni kuhusu tangazo langu la Jumamosi. Msiwe na hofu suala hili ni la hiari,`` alisema.

  Aliendelea kuwasisitiza Wabunge kushiriki ipasavyo katika zoezi hilo ikiwa ni hatua za kumuunga mkono Rais na kwamba yeye (Spika) atakuwa wa kwanza.

  Kazi ya upimaji itatanguliwa na mbio za wabunge na mawaziri ambazo zitapokelewa na Waziri Mkuu kwenye viwanja vya Bunge kesho.

  Pamoja na Spika kuwataka wabunge wasiwe na udhuru kesho, Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Bw. Ibrahim Mohamed Sanya alimuaga Spika kwamba anadharura ya kwenda Morogoro kesho hivyo hatashiriki kwenye upimaji huo.

  Ombi hilo lilisababisha kuangua kwa vicheko kwa Wabunge na wageni wanaosikiliza Bunge jana asubuhi.

  Akifafanua zaidi, Spika alisema ingawa suala la kupima Ukimwi ni la hiari lakini kwa kiongozi wa kisiasa kukwepa linaweza kuleta matatizo kisiasa.

  Kwa mujibu wa Spika, Bunge lililopita Mwaka 2000 walipopima Ukimwi walijitokeza wabunge 20 tu.

  * SOURCE: Nipashe

  ReplyDelete
 7. Wazee wetu nao kwa acrobats zakimiujiza hawajambo yaelekea ukiwa kwenye nafasi kule Tanzania una ruksa ya kuunda sheria? peke yako.

  ReplyDelete
 8. Mija, huwa napitia na ingawa sisemi, ningependa kujua vitu nane kukuhusu.
  http://serinaserina.wordpress.com/2007/07/23/vitu-nane-msizojua-kunhusu/

  ReplyDelete
 9. Damija,
  Salaam kutoka mashariki ya mbali.
  Hii blog yako ni nzuri na mara nyingi ina maoni mazuri sana.
  Lakini hizi background colours
  naona kama zipo dark kiasi. Kila niingiapo kwenye blog yako nahisi kama nakutana na kiza. Nadhani wakina-dada ni wachaguzi wazuri sana wa rangi. Kwa hiyo najua hilo halikupi taabu. Asante.

  ReplyDelete
 10. Wabunge wamgeuka Spika

  na Martin Malera, Dodoma


  BAADHI ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameanza kuonyesha shaka dhidi ya utendaji kazi wa Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

  Shaka kubwa waliyoionyesha, ni kuhusu uwezo wake kama Spika wa Bunge katika kusimamia hoja za wabunge na kuzitolea maamuzi.

  Ingawa kumekuwa na manung’uniko ya chini chini dhidi ya mwenendo wa Spika Sitta kulingana na ahadi zake kabla na baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo, hali hiyo sasa inaonekana kwenda mbali zaidi, baada ya Mbunge wa Manyoni Magharibi, John Lwanji (CCM), kutamka bayana bungeni kuwa, Spika Sitta anaacha hewani hoja nyingi za muhimu.

  Akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya makadirio ya matumizi na mapato ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha wa 2007/2008, iliyowasilishwa bungeni juzi na Waziri Zakhia Meghji, Lwanji alisema anatamani Bunge liwe na Spika kutoka nje ya Bunge, tofauti na sasa ambapo ni mmoja kati ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano.

  Alisema hali hiyo inatokana na kiti cha Spika (kwa sasa Samuel John Sitta) kuacha hoja nyingi za muhimu za baadhi ya wabunge, akiwemo yeye, bila kutolewa majibu ya uhakika wala kupatiwa ufumbuzi.

  Akizungumzia masuala hayo aliyoyaita muhimu ambayo hayajapatiwa ufumbuzi, Lwanji alisema katika jimbo lake kuna tatizo la simba wala watu na hadi juzi wakati anatoa hoja hiyo, mtu mmoja aliripotiwa kuliwa na simba na kubakizwa kichwa ambacho kilizikwa juzi hiyo hiyo.

  Alisema mtu huyo alikuwa akitoka katika moja ya vijiji vya Wilaya ya Manyoni kwenda mjini kwa ajili ya kupata huduma za kibenki, na akiwa njiani akiendesha baiskeli, alivamiwa na simba.

  Lwanji alieleza kuwa, tatizo la simba wala watu katika wilaya hiyo ni la muda mrefu, na alishaliwasilisha bungeni, lakini hadi sasa halijapatiwa majibu na hata kiti cha Spika kimeliacha tatizo hilo pasipo majibu.

  “Manyoni tuna tatizo la benki, watu wanatoka mbali kuja mjini kupata huduma za benki ya NMB, njiani wanakumbana na simba wala watu, nilishatoa malalamiko hapa, hakuna majibu, na Spika ameacha jambo hilo bila kupatiwa majibu.

  “Mimi nadhani katiba inaruhusu Spika kutoka nje ya Bunge, labda tunaweza kupata majibu yetu kwa ufasaha, lakini tuliona busara tuwe na Spika kutoka ndani ya Bunge…,” alisema Lwanji.

  Wakati akiendelea kulalamikia suala la Spika, Naibu Spika Anna Makinda aliingilia kati na kumtaka mbunge huyo kuwasilisha malalamiko yake katika taratibu zinazotakiwa, na kumtaka aelekeze hoja yake katika wizara iliyokuwa mbele yake.

  Lwanji aliendelea, tatizo hilo la simba wala watu katika jimbo lake kuwa lina athari zake kiuchumi, kwamba idadi kubwa ya mifugo inaliwa na simba kila mwaka jambo linalorudisha nyuma juhudi za wananchi wa eneo hilo za kusonga mbele kiuchumi.

  Aliitaka Wizara ya Fedha kuhakikisha huduma za benki ya NMB zinawafikia wananchi ili kuwaondolea urasimu wa NMB Manyoni pamoja na kuwaepusha na tatizo la simba.

  Baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili juzi katika viwanja vya Bunge, walieleza kuwa Spika Sitta atakabiliana na wakati mgumu katika kutekeleza ahadi zake kwa Watanzania wenye shauku ya kuona mabadiliko aliyoyaahidi baada ya kuyakosa kwa muda mrefu.

  Wabunge hao ambao waliomba majina yao yasitajwe, walieleza kuwa Watanzania wengi sasa wanapata habari za Bunge baada ya vyombo vya habari kuanza kurusha moja kwa moja vikao vyake kupitia redio na televisheni.

  Kwamba kushindwa kwa Spika kuchukua hatua hata katika masuala ambayo yalikuwa yakilidhalilisha Bunge, ni moja ya mambo ambayo yanapunguza imani ya wananchi dhidi ya Spika kwa kuzingatia ahadi zake alizotoa awali.

  Hii si mara ya kwanza Spika Sitta kupingwa hadharani kuhusu mwenendo wa utendaji wake. Mara ya kwanza ni mapema mwaka jana wakati Watanzania wengi walipomshambulia baada ya kutangaza nia yake ya kupigania nyongeza ya mishahara na marupurupu ya wabunge wakati taifa likiwa katika baa la njaa na tatizo la mgawo wa umeme.

  Aidha, Sitta pia alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuibuka malumbano kati yake na mbunge kijana wa CCM, Adam Malima, aliyefikia hatua ya kumshitaki kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

  Wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa walieleza kuwa, Spika Sitta aliamua kutopambana wala kutomuadhibu Malima hata baada ya kubainika kuwa alilidanganya Bunge, kwa kuhofia kupokwa wadhifa wake na kundi la wanamtandao, ambalo linadaiwa lilikuwa limekwishaanza kumtazama kwa jicho la kumuengea.

  Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, juzi alishindwa kujibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini, Siraji Kaboyonga (CCM), aliyetaka kujua fedha za ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Twin Tower, zilikotoka.

  Kaboyonga alisema gharama za ujenzi wa Twin Tower hazilingani na thamani ya mtaji wa BoT, hivyo, alihoji mahala zilipopatikana fedha za ujenzi huo, unaolalamikiwa kwa muda mrefu sasa.

  Aliposimama kujibu swali hilo, Meghji alijikuta akitoa taarifa ya uchunguzi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akieleza kwamba umebaini kuwa ujenzi wa majengo hayo hauna matatizo kama inavyodhaniwa.

  Wakati anakaa kwenye kiti chake, Kaboyonga alirejea tena swali lake. “Nafikiri waziri hajajua swali langu, nasema hivi, mtaji wa BoT ni sh bilioni 20, lakini thamani ya majengo yake, haiendani na mtaji huo, fedha hizo za ujenzi zimetoka wapi?”

  Kabla ya Meghji kujibu, Naibu Spika, Anna Makinda, aliingilia kati na akatangaza kuafikiwa kwa kifungu hicho na baadhi ya wabunge kuitikia ‘ndiyo’.

  Hata hivyo, katika kujaribu kuondoa kadhia hiyo, baadhi ya maofisa wa BoT waliokuwepo bungeni, walilazimika kutoa majibu ya ziada ambayo Waziri Meghji baadaye aliyasoma bungeni.

  Akisoma majibu hayo, Meghji alisema fedha za ujenzi wa Twin Tower zimetokana na faida ya muda mrefu ambayo BoT ilikuwa imejiwekea.

  Hata hivyo, hakutaja kiasi cha fedha kilicholimbikizwa hadi kujenga majengo hayo.

  ReplyDelete
 11. Spika Sitta, rejea ahadi zako  MATARAJIO ya wabunge na Watanzania kwa ujumla kuhusu azma ya Spika wa Bunge, Samuel John Sitta ya kurejesha hadhi ya Bunge, sasa yanaonekana kutoweka.

  Wengi hawaamini kama ni Sitta huyu ambaye wakati akiomba kuchaguliwa kushika wadhifa huo na hata baada ya kuchaguliwa, alikuwa akijigamba kuliongoza Bunge kuelekea katika mabadiliko makubwa ya kuwa na hadhi inayostahili, ambayo si siri kwamba enzi za utawala wa awamu ya tatu ilitoweka.

  Kwamba, huyu ndiye Spika Sitta aliyekuwa akijigamba kuwa ni Spika wa ‘Standard and Speed’, ambaye mara tu baada ya kuchaguliwa, aliwataka mawaziri wakae chonjo dhidi ya majibu yao ya ubabaishaji kwa wabunge.

  Kinyume chake, ikiwa ni takriban miaka miwili tangu aliposhika wadhifa huo, matendo yake kama kiongozi wa Bunge kulingana na ahadi zake, yanaonekana kuwa kinyume kabisa.

  Haina shaka kwamba, wananchi waliokuwa wakisubiri kuona utekelezwaji wa ahadi alizozitoa, wana mengi ya kuzungumza kuhusu Spika Sitta, kinachowatatiza ni kukosa mahali pa kutolea dukuduku lao.

  Lakini wabunge, ambao wanayo sehemu ya kusemea, wameanza kutoa dukuduku lao kuhusu utendaji kazi wa Sitta kama Spika wa Bunge.

  Hili linathibitishwa na kauli ya Mbunge wa Manyoni Magharibi, John Lwanji (CCM), aliyoitoa juzi bungeni kuwa, anatamani Spika wa Bunge angekuwa si mbunge, tofauti na sasa ambapo ni mmoja kati ya wabunge.

  Lwanji ameeleza wazi kuwa, tamaa yake hiyo inatokana na Spika wa sasa, Samuel Sitta, kuacha hoja nyingi za muhimu za baadhi ya wabunge, akiwemo yeye, bila kutolewa majibu ya uhakika wala kupatiwa ufumbuzi.

  Lwanji si wa kwanza kuonyesha dukuduku la aina hii dhidi ya Spika. Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, Spika Sitta alianza kupingwa na Watanzania siku chache tu baada ya kukalia kiti hicho, pale alipotangaza nia yake ya kupigania ongezeko la mishahara na marupurupu ya wabunge katika kipindi ambacho nchi ilikuwa na matatizo makubwa ya baa la njaa.

  Hata hivyo, azma hiyo ya Spika Sitta, imefanikiwa hivi karibuni baada ya serikali kuamua kuongeza mishahara na marupurupu ya wabunge, huku ikiwaacha Watanzania wengine, hasa wenye kipato cha chini, wakiendelea kusongwa na ugumu wa maisha kwa kuruhusu mfumuko wa bei. Katika hili amefanikiwa!

  La kwanza lilionyesha shaka dhidi ya uwezo wa Spika Sitta katika kutekeleza ahadi zake nyingine ni pale alipoingia katika mgogoro na Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima, ambaye alikataa kwenda ofisini kwake kwa ajili ya usuluhishi.

  Spika aliwashangaza Watanzania pale aliposhindwa kumshughulikia Malima, hata baada ya kubainika kuwa alilidanganya Bunge na kwa makusudi akaamua kumshitaki katika chama chake, akieleza kuwa ndani ya chama, Spika ni sawa na Malima.

  Ingawa inaelezwa kuwa Spika Sitta alimgwaya Malima kwa sababu alikuwa akikingiwa kifua na viongozi wengine wakubwa serikalini, ambao walikuwa na mkakati wa kumvua madaraka yake, lakini sisi tunadhani hapo ndipo alipaswa kuonyesha msimamo wake kwa vitendo, navyo si vingine, bali kumshughulikia Malima ambaye alikuwa amelidhalilisha Bunge.

  Si nia wala kazi yetu kumfundisha Spika Sitta jinsi ya kutekeleza majukumu yake, lakini kama sehemu ya Watanzania, tunao wajibu kumshauri, hasa pale tunapoona inafaa.

  Na ushauri wetu kwake ni kwamba, ni vizuri awe makini na ahadi zake, vinginevyo, u-Spika utakuwa mzigo mzito, unaoweza kumwekea rekodi mbaya ya utendaji wake. Hivyo, itakuwa busara akirejea ahadi zake.

  ReplyDelete
 12. Tunashukuru sana kwa kututembelea karibu sana tena sana.
  Wengine nao tunaomba muwe mnatutembelea.
  Karibu sana Kijiweni

  ReplyDelete
 13. Bunge bado halijapata Spika wa Viwango na Kasi
  Absalom Kibanda


  SAMWEL Sitta ni mwanasiasa mwenye mbwembwe nyingi. Kwa wanaomfahamu, wanasema amekuwa hivyo tangu akiwa kijana mdogo, hata kabla hajateuliwa kuwa waziri zama za Serikali ya Awamu ya Pili.

  Kwetu sisi tuliomfahamu akiwa mtu mzima na hasa tangu alipoteuliwa na chama chake kuwa mgombea uspika na baadaye akashinda kwa kura nyingi, ni mashahidi wa kweli wa namna alivyo mwanasiasa mwenye mbwembwe nyingi.

  Aliposhika nafasi hiyo mwishoni mwa mwaka 2005, Sitta kama walivyopata kufanya viongozi wengine wakuu baada yake, Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alikuja na misamiati mitamu masikioni.

  Huku akijua kuwa, Rais Kikwete alikuwa ameingia kwa gia ya Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya, yeye aliamua kuifanyia marekebisho kidogo kaulimbiu hiyo ya mkuu wa wanamtandao, na akaliambia Bunge kuwa eti angelikuwa Spika wa Standard and Speed (Viwango na Kasi).

  Siku alipowatangazia wabunge kuwa huo ndiyo ungekuwa mwongozo wake wa kazi wakati atakapokuwa Spika wa Bunge, ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe, pande zote mbili, ule wa CCM na wapinzani zikaonekana kumuunga mkono.

  Mbwembwe za Sitta hazikuishia hapo, kwani alisonga mbele zaidi na siku zake za mwanzo akaonekana akijaribu kuwa msumari wa moto kwa wabunge wa pande zote mbili, pasipo kujali tofauti za kichama.

  Siku chache baadaye, wakati wa kikao cha kwanza cha Bunge akiwa Spika, Sitta akalitangazia Bunge hilo kuwa, kanuni nyingi za Bunge zilikuwa zimepitwa na wakati na akaahidi kulifanyia jambo hili marekebisho ya haraka ili kuifanya taasisi hiyo ifanye kazi zake chini ya falsafa yake hiyo ya Viwango na Kasi.

  Kwa mara ya kwanza, ndani na nje ya Bunge, Sitta akaanza kuonekana kuwa shujaa wa mabadiliko ya kibunge, kiasi cha kumfanya aonekane kuwa mtu makini zaidi kuliko alivyopata kuwa mtangulizi wake, Pius Msekwa.

  Ahadi za kuwa Spika wa Viwango na Kasi, kuzifanyia mabadiliko kanuni za Bunge na ahadi yake kwamba angetumia zaidi ‘common sense’, yaani akili za kuzaliwa badala ya kanuni hizo zilizopitwa na wakati, zilipokewa kwa shangwe na wananchi wengi ambao walikuwa wameanza kupoteza imani na Bunge, ambalo lilianza kuonekana kuwa ni taasisi mahususi ya kuilinda na kuibeba serikali kwa gharama zozote zile zama za uspika wa Msekwa.

  Hatua hizo za Sitta kimsingi ziliwafanya baadhi ya wananchi na hata wabunge wa upinzani kwa mara ya kwanza kuanza kukubali kuwa, uteuzi wa mwanasiasa huyo kushika wadhifa wa juu katika Bunge ulikuwa ni sahihi kabisa na ambao kwa hakika haukuwa na tone la walakini.

  Mara moja, Sitta alianza kuonekana kuwa mwanasiasa mapinduzi na mtu aliyekuwa tayari hata kupoteza uanachama wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu ya kuwatetea wabunge wao au kulinda hadhi ya Bunge.

  Taswira hiyo isiyo halisi, ilisababisha wabunge, wakiwamo wale walioonekana kuwa makini kutoka katika kambi ya upinzani, kumuunga mkono kwa nguvu zao zote, kiasi cha kutusakama hata sisi wanahabari ambao wakati fulani fulani tulionekana kumhoji-hoji Spika kipenzi chao. Walikuwa wamekosea.

  Baadhi ya wabunge hao walifikia hatua ya kutuasa wanahabari kufanya kila linalowezekana, kumsaidia ‘Spika wao’ dhidi ya kile walichokuwa wakikiita vita kali aliyokuwa akipigwa na viongozi wenzake wakuu ndani ya CCM, eti kwa sababu ya msimamo wake thabiti. Hili lilikuwa kosa jingine.

  Kwa mara ya kwanza, baadhi ya wananchi waliokuwa wamehadaika na ushawishi wa kishabiki wa sisi wanahabari na wabunge waliokuwa wakimpamba, walianza kupata wasiwasi kuhusu mwanasiasa huyo, wakati alipojitokeza hadharani na kupigania kwa nguvu maslahi ya wabunge, wakati akijua kuwa, wafanyakazi wa kada nyingine katika sekta ya umma walikuwa wakikabiliwa na ukata mkali wa kimaisha kuliko ule wa kisiasa wa wabunge.

  Kama hiyo haitoshi, baadhi yetu tulianza kuingiwa na wasiwasi wa uwezo wake wa kimaamuzi na kimatendo, pale alipoonyesha dhahiri kushindwa kwake kuwaruhusu wabunge waiangike Kampuni ya Richmond, baada ya kilio dhidi yake kuonekana kikiongezeka kila kukicha.

  Udhaifu wake kama Spika haukuishia katika suala hilo tu, bali ukweli mbele zaidi wakati alipokubali zaidi ya shilingi milioni 100 za walipakodi ziteketee hivi hivi katika shauri lililomhusu Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima na mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi.

  Uamuzi wake wa kulimaliza suala hilo kwa njia ya kile alichokiita kuwapatanisha watu hao, hata baada ya Kamati ya Bunge kubaini kuwa Malima alikuwa amesema uongo bungeni wakati akimtuhumu Mengi kulipokewa kwa mshangao mkubwa na baadhi yetu.

  Hata hivyo kwa watu wanaofahamu utendaji wa CCM na msingi mkuu wa chama hicho kumfanya Spika anayetokana na chama chao hicho kuwa mjumbe wa Kamati Kuu yake, hawakupata shida kubaini sababu za Sitta kufanya hivyo. Alikuwa ameamua kukilinda chama chake.

  Sisi wa Tanzania Daima, kwa makusudi kabisa tuliamua kuziba masikio na tukaeleza bayana kusikitishwa kwetu na uamuzi huo wa Sitta, tukiueleza kuwa uliojaa utatanishi na kuacha maswali mengi kuliko majibu.

  Tangu wakati huo na hata kabla ya hapo, binafsi nilianza kumuangalia Sitta kuwa aina ya wanasiasa wa CCM ambao wamekuwa wakiingia madarakani wakiwa na mbwembwe nyingi na kujikuta wakilowa muda mfupi baada ya kukabiliwa na msumari wa moto wa vikao vikali vya chama hicho.

  Ushahidi wa hili ni rahisi kabisa. Leo hii, Sitta ameanza kudhihirisha hilo. Ni dhahiri kuwa, CCM imemshinda nguvu na sasa jeuri ya kuitumia ipasavyo kaulimbiu yake ya Viwango na Kasi, haiwezekani kufanya kazi ipasavyo pengine kama ni kwa matakwa ya CCM.

  Sitta kwa mara nyingine tena alionyesha, u-CCM wake jana wakati wa mjadala wa hoja binafsi ya Kabwe Zubeir Zitto, iliyokuwa ikipendekeza kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kumchunguza Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi aliyesaini mkataba mpya London, Uingereza.

  Spika ambaye ndiye aliyekuwa akiongoza mjadala huo, kwa namna ya pekee kabisa alionekana kuwa mkali kweli kweli kila mara wabunge wa upinzani walipokuwa wakichangia mjadala huo.

  Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, alikuwa anaweza kuona waziwazi namna Sitta alivyojaribu bila ya mafanikio kujenga mazingira ya hoja hiyo kuchukua mtazamo wa kivyama zaidi, ajenda iliyokuwa mezani kwake.

  Naamini kwa mara ya kwanza kuanzia jana, wabunge wa upinzani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimuona Sitta kuwa rafiki wao wa kweli eti tu kwa sababu ya kuwatega kwa kuwapa fursa ya kuwasilisha hoja binafsi, sasa wataweza kujionea wenyewe namna CCM kwa mara nyingi tena ilivyolinyima Bunge kupata aina ya Spika waliyemhitaji.

  Watanzania hawana budi kusubiri hadi hapo Sheria ya Wagombea Binafsi itakapoanza kutumia kabla hawajaanza kuwa na Spika wa Bunge ambaye atakuwa na ubavu wa kusema na kuyasimamia kwa vitendo maneno yake. Huko ndiko tuendako.

  0786 729 999
  absakib@yahoo.com

  ReplyDelete
 14. Spika Sitta; hizi ni alama za nyakati
  Ndeonasia Meero


  “NIMETIMIZA wajibu wangu, moyo wangu ni mweupe, naliachia bunge lifanye kazi yake, maamuzi ni ya Bunge.” Haya ni maneno aliyosema Mheshimiwa Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) muda mfupi kabla ya kusimamishwa kazi ya ubunge.

  Zitto, alikuwa tayari kwa maamuzi yoyote ambayo Bunge litachukua juu yake kuhusu hoja binafsi aliyoiwasilisha akitaka uchunguzi wa kina ufanyike na iundwe kamati maalum ya Bunge ili kujua kilichosababisha Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kusaini mkataba wa madini nje ya nchi.

  Zitto, alifanya hivyo kwa niaba ya Watanzania wote na si wananchi wa Kigoma Kaskazini pekee.

  Alifanya hivyo kulinda maslahi ya nchi na kujiridhisha kwamba watawala wa awamu ya nne hawaendi kinyume na kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuhakikisha mikataba yote ya madini yenye utata inapitiwa na kurekebishwa.

  Zitto, ni mbunge wa upinzani. Sisi ni mashahidi kwamba idadi ya wawakilishi wa upinzani ndani ya Bunge la Jamhuri hazidi robo ya wabunge wote. Zitto, mbunge kijana, mwanasiasa machachari, anayejua kujenga na kutetea hoja zake, alinyimwa haki yake ndani ya jumba la kutunga na kupitisha sheria.

  Waliposhikilia wanaCCM hao ni kwamba mwenzao (Karamagi) si mwongo, wanajiridhisha kwa hotuba yake iliyojaa mbwembwe, tashititi na tambo zisizo na majibu sahihi ya hoja ya Zitto. Ni vipi wanaCCM hawa wanakuwa miungu-watu wenye kujua nani mkweli na nani mwongo bila kuchunguza?

  Walioshiriki kumkandamiza Zitto, walifanya hivyo kwa makusudi. Walikuwa wasemaji wa serikali, kazi ambayo waliyoikurupukia kulinda maslahi zao na kusahau kuwa wapo pale kwa ajili ya wananchi.

  Sisi wananchi ndiyo tuliowaajiri wote waliojifanya kimbelembele kuhakikisha hakuna kamati itakayoundwa ili kujua ukweli wa mambo.

  Nashangaa na kujiuliza kwamba hawa wabunge wanatufanya wananchi kama watoto wasio na uwezo wa haraka kubaini mambo. Ni kweli si wote wanaojua kanuni za Bunge, lakini kejeli na kashfa walizoonyesha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliosimama kidedea kuhakikisha hakuna kamati itakayoundwa, ilitupa majibu ya moja kwa moja.

  Nilishangaa na kustaajabu kauli alizotoa Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima kuhusu hoja hiyo, anataka tumwone kuwa yeye ni msafi na mwadilifu sana bungeni? Amesahau alivyopoteza sh milioni 100 za wauza karanga na mchicha kwa uongo wake?

  Alithubutu kupeleka mashahidi wa uongo kwenye kamati iliyoundwa na Bunge kwa ajili ya kuchunguza mgogoro dhidi yake na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.

  Hivi Malima, umeyasahau haya ndani ya kipindi kifupi kweli au ulitaka wapigakura wako wakuone ulipokuwa unazungumza? Niwie radhi kama kauli hizi zitakuwa kali kwako na waajiri wako (wananchi wa Mkuranga).

  Katika hili la Malima, Spika alithibitisha kwamba mashahidi na vielelezo vilivyotolewa na mbunge huyo havikuwa na ukweli ndani yake. Kwa busara za Spika hakumwadhibu msema uongo pamoja na jeuri iliyoonyeshwa na Malima kwa Bunge na Spika, lakini alisamehewa kwa vile hajui alilolitenda.

  Spika alisema haya wakati fedha za Watanzania na muda wa waheshimiwa ulishapotea katika suala la uongo. Anyway, muda si tatizo, bali fedha za walipa kodi maskini Watanzania sisi zinaliwa ili kuthibitisha uongo. Kizuri zaidi uamuzi wa suluhu kati ya Mengi na Malima hujatekelezwa hadi leo, sababu anaijua Spika.

  Sikupenda kwenda mbali, lakini kilichofanyika Agosti 15, mwaka huu ndani ya Bunge ilikuwa ni kupindisha sheria, kumnyima haki Zitto kutokana na tofauti yake kiitikadi, wana CCM wakaweka utaifa kwapani na kushabikia wasichokijua ama walichokijua kwa maslahi ya waliowatuma kufanya hivyo. Wanawatukuza sana hao na kuwaita wawekezaji.

  Huyu Mudhihir Mudhihir, Mbunge wa Mchinga, binafsi namuita mamluki. Hakujua alichosema, alifurahia kupewa nafasi, lakini hakutafakari kwa kina kabla ya kuzungumza.

  Siku ile wangekuwepo bungeni waliompigia kura, wangemtendea haki kwa sababu walichomtuma hakutekeleza, matokeo yake anashabikia kutoundwa kwa kamati ya kuchunguza namna Tanzania ilivyotia saini mkataba wa madini nchini Uingereza.

  “Mheshimiwa Spika, niliipenda sana hekima yako ya kumtaka mheshimiwa Zitto kama ana lolote aseme, nilijua kwa utu uzima wako, ulikuwa unakusudia nini. Kwa bahati mbaya sana amesema yeye ni Democrat, litakalotokea na litokee. Katika mazingira kama hayo, mimi nashindwa kubadilisha msimamo wangu. (msimamo wake ni kusimamishwa uwakilishi chini ya Kanuni ya 59(iii) kwa kipindi chote cha kikao cha Bunge la nane na tisa),” alisema Mudhihir.

  Mudhihir, alimaliza kwa kuwashukuru wanaCCM wote waliochangia kisha aliyemeza maamuzi yake kwa kuwa hakuwa na njia nyingine ya kusaidia heshima ya jimbo lake.

  Sitaki kuamini kuwa wabunge wa CCM walipoteza muda mwingi kushabikia namna ya kuficha ukweli kwa maslahi ya wananchi wote, nahisi hawa si wenzetu hata kidogo, wanatuelekeza kwenye keki ya ugumu wa maisha huku wakijihakikishia maisha bora zaidi toka kwa wanaowaita wao kuwa ni wawekezaji.

  Kila nikiikumbuka siku hiyo na kuwatafakari wabunge wa CCM nabaki kinywa wazi. Nikifikiria kauli za John Malecela yule Mbunge wa Mtera, napata jibu kuwa kuenguliwa kwake katika kinyang’anyiro cha urais ilikuwa halali kabisa. Kwa umri aliokuwa nao, naamini alishaona mengi, lakini katika hili, mheshimiwa huyu aliamua kufumba macho.

  Baada ya wanaCCM watiifu kushinikiza kutoundwa kwa kamati ya kuchunguza nani mkweli kati ya Karamagi na Zitto, Spika alihitimisha kwa kupiga kura. Kama ilivyo ada wenyewe wanaita demokrasia, wanaCCm hao wakapaza sauti ya ‘NDIYOOOO’ iliyomeza ‘HAPANA’ ya wapinzani.

  Spika aliahirisha Bunge saa 2:05 usiku na wote walijipongeza kwa uamuzi wao. Waliwasahu waliowachagua na ukweli kuhusu mwenendo wa madini nchini. Hizi ni alama za nyakati, kinachofuata ni kuwanyima ajira wabunge wote wa CCM.

  Sitaki kuwazungumzia wote waliochangia, si kwa sababu ya wingi wao, la hasha bali kwa sababu ya ufinyu wa nafasi gazetini.

  Waswahili husema, wengi wape, lakini katika hili linalogusa maslahi ya taifa, Spika angalia upya maamuzi yako wananchi tupo tayari kodi zetu zitumike ili mwongo ajulikane kati ya Zitto na Karamagi.

  Mwandishi wa makala hii amejitambulisha kuwa ni msomaji wa gazeti hili anayepatikana kwa anwani ya S . L. P 71593, Dar es Salaam.

  ReplyDelete
 15. Ninampenda Spika Samuel Sitta
  Charles Mullinda


  NINAMPENDA sana Spika Samuel Sitta, wallah naapa! Ninampenda kwa sababu hafichi uwezo wake wa utendaji kazi kama kiranja wa Bunge letu.

  Ninaipenda sana kauli aliyoitoa siku chache baada ya kuapishwa kuwa kiranja wa Bunge, kwamba ataliongoza Bunge kwa ‘Standard and Speed’, yaani viwango na kasi.

  Siku aliyotamka bila wasiwasi kwamba anakusudia kupigania maslahi zaidi kwa ajili ya wabunge, nilimfurahia sana kwa sababu niliweza kumfahamu jinsi alivyo.

  Alisema hivyo katika ukumbi wa mikutano wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam. Nilichogundua kwake baada ya kauli hiyo ni kwamba, Spika Sitta ni kiongozi mbinafsi, asiyewajali watu wake, anayetaka kuongezewa yeye tu, bila kujali kama kuna wengine wenye uhitaji wa lazima wa kuongezewa walau kidogo ili wafikie hata robo ya kile anachokipata yeye.

  Nilimpenda sana alivyotamka kile kilichokuwa moyoni mwake bila kuficha, nilifurahi kuelewa kuwa yeye hana habari ya baa la njaa lililokuwa likiwakabili Watanzania, hana habari ya tatizo la mgawo wa umeme, hana habari na ukame, kilichokuwa akilini mwake yeye na wabunge wenzake, ni kuongezewa mishahara na marupurupu ili wawe kama wabunge wa nchi nyingine ambazo uchumi wake uko juu.

  Ninampenda Spika Sitta kwa sababu ana huruma na anawapenda wabunge wa CCM wanaolidanganya Bunge, huwa anawahurumia na kuomba wapewe ushauri nasaha. Jamani mimi nampenda Spika Sitta, wallah naapa, ninampenda yeye na mbwembwe zake.

  Fikiria, Spika wa ‘Standard and Speed’ anashitakiwa na mbunge ambaye amefanya kosa la kulidanganya Bunge kwa katibu mkuu wa chama cha siasa, mbunge huyo anakataa kwenda ofisini kwa Spika, na anapopigiwa simu na Spika, anaamua kuizima kabisa, hataki usumbufu, halafu Spika kwa busara zake, anawaomba wabunge wampe ushauri nasaha, huu ni upendo mkubwa kutoka kwa Spika wetu.

  Kama kuna mtu anamchukia Spika Sitta kwa maamuzi yake yenye utata katika sakata la Malima na Mengi mimi sitamuelewa. Si tunakumbuka Spika Sitta alisema kwamba ‘kati ya Malima na Mengi hakuna aliyeibuka mshindi katika kesi yao’? Kwa maana nyingine walitoka suluhu bin suluhu!

  Naamini mnakumbuka ile kauli ya Spika kwamba, ‘watu wengi walitarajia kuona mtu mmoja akiibuka mshindi na mwingine akishindwa na kupewa adhabu, lakini haitakuwa hivyo.’ Na kweli haikuwa hivyo.

  Spika ana maamuzi yake ambayo mara nyingi yanakuwa kinyume kabisa na matarajio ya Watanzania, hataki kuwa mtu wa kutabirika. Mnapodhani kuna kosa linalostahili adhabu ili iwe fundisho kwa wakosaji wengine, yeye kwa kutumia busara zake, badala ya kanuni, anaamua kusamehe na kutoa ushauri nasaha.

  Spika wetu ni mtu aliye wazi, alijua kabisa kuwa mamilioni ya fedha za Watanzania yametumika katika sakata la Malima na Mengi na Kamati ya Bunge ilithibitisha Malima alilidanganya Bunge, lakini busara za Spika zilimuongoza kwamba, Malima alipaswa kuonewa huruma zaidi kuliko jasho la Watanzania maskini, ndivyo ilivyo na wala hakuficha, alisema hivyo bungeni!

  Spika ni mtu wa ‘surprise’, wakati inapodhaniwa kuwa atatumia busara zake za u-Spika, hazitumii, lakini wakati usiotarajiwa, anazitumia. Jiulize, kwa nini hakutumia busara zake mapema kuwapatanisha Malima na Mengi kabla taifa halijapoteza sh milioni 100 kwa kuketi vikao 60 kwa ajili ya kusikiliza shitaka hilo? Utaelewa ni wakati gani Spika huwa anajisikia kutumia busara zake.

  Watanzania watakubaliana na mimi kuwa, Spika Sitta hatabiriki. Niwakumbushe ‘issue’ ya Chitalilo, yule mbunge wa Buchosa anayedaiwa kughushi vyeti vya elimu yake.

  Si mnakumbuka jinsi Spika Sitta alivyochanganya habari? Kwanza alikaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa mbunge yeyote atakayebainika kughushi vyeti vya elimu yake, atachukuliwa hatua zinazostahili kwa sababu ubunge haumfanyi mtu kuwa juu ya sheria.

  Halafu baadaye kidogo, upelelezi wa polisi ulipokamilika na kuthibitisha kuwa ni kweli Chitalilo alighushi vyeti vya elimu yake, akawa bubu. Hakutaka tena kuliongea suala hilo, yaani Spika bwana, anafurahisha kweli kweli!

  Sasa angalia jinsi Spika alivyo na busara, naamini lile sekeseke lililoibuliwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto kuhusu kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa Buzwagi huko London, Uingereza halijasahaulika, hivyo tunakumbuka vizuri uamuzi wa Spika katika suala hilo.

  Zitto alifunua uozo wa kusainiwa kwa mkataba huo nje ya nchi, pamoja na vikorokoro vingine vingi vya hovyo katika sekta hiyo. Serikali ikajaribu kutoa maelezo yake, lakini Zitto, kijana mpambanaji hakuridhika na majibu ya serikali, akaenda mbali zaidi, akaanza maandalizi ya kuwasilisha hoja binafsi ya kulitaka Bunge kuunda kamati teule ya kuchunguza sekeseke hilo, Spika akiwa anajua fika kuhusu hilo.

  Zitto akaiwasilisha hoja hiyo, Waziri Karamagi akajaribu kujibu huku ‘akilia’ kwa kuchafuliwa jina, huku akimtupia makombora mazito yaliyokuwa yakichafua jina lake, Spika akiwa katika kiti chake cha enzi akisikiliza sakata zima.

  Wabunge wa CCM walipoona serikali inataka kushikwa pabaya, wakaamua kufanya walichokifanya, huku wakijua kuwa kilio cha wananchi dhidi ya sekta ya madini ni cha muda mrefu na hadi sasa hakijapatiwa majibu.

  Wakaungana kukataa kuundwa kwa kamati teule ya kuchunguza jambo hilo, ambalo hata kama lilisainiwa kwa nia njema, usiri na uharaka wake bado unatia shaka kwa sababu bila Zitto kuwaeleza Watanzania kuhusu kusainiwa kwa mkataba huo, wengi wangebaki gizani.

  Inaelezwa kwamba, tangu asubuhi ya siku ya Jumanne, ilikwishafahamika kuwa Zitto atasimamishwa ubunge kwa kosa ambalo mpaka sasa linatiliwa shaka na wengi, lakini Spika, ambaye mara zote hutumia zaidi busara katika maamuzi yake, wala hakuhangaika kumuita Zitto na kumuasa kwa busara zake kuhusu nia yake ya kuwasilisha hoja yake binafsi.

  Ila, kwa kutumia busara zake katika suala kubwa kama hili, huku akitambua kuwa hata Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwa nyakati tofauti wakiwa ndani na nje ya nchi wamekwishakaririwa wakizungumzia tatizo la mikataba ya madini na kusisitiza haja ya mikataba hiyo kufanyiwa marekebisho, akaona hakuna haja ya kuundwa kwa kamati teule.

  Nadhani wanapaswa kutafakari namna nzuri ya kufikia maamuzi, kama ni kufuata kanuni au busara za kawaida za mtu.

  Watafakari kama kulikuwa na umuhimu wa kuunda kamati katika sakata la Malima na Mengi, lakini katika hili linalogusa rasilimali za nchi yetu, kuundwa kwa kamati kunategemea matakwa ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi!

  Jambo linalonifanya niendelee kumpenda Spika, pamoja na mambo yote haya, ni jinsi anavyonufaisha pande zote anazoziongoza. Spika kwa nia njema kabisa ameamua kuwahadaa wanaCCM wenzake kwa kumuadhibu Zitto wanayedai kuwa anajitafutia umaarufu wa rejareja, huku akijua kuwa kufanya hivyo, ndiyo kabisa kunaongeza umaarufu wa Zitto.

  Angalia sasa suala hilo limekwishadakwa na wanaharakati, wanasheria, wananchi na sasa umaarufu wa Zitto ni mkubwa kwelikweli kuliko wa Karamagi, na ninadhani kuliko hata wa Spika mwenyewe. Kwa haya yote, ndio maana mimi nampenda Spika Samuel Sitta.

  0734 – 00 35 12
  cmullinda@yahoo.com

  ReplyDelete
 16. Kimya Kingi kina Mshindo.
  Tumeona picha za shughuli kule kwa Mjengwa. Hongereni sana!
  Kila la Kheri.

  ReplyDelete
 17. Da Mija pole na shughuli.Hongera sana Da Mija.Jamani umependeza

  ReplyDelete
 18. HONGERA KWA KUFUNGA NDOA DA' MIJA!!!

  ReplyDelete
 19. <a href="http://medonlineshops.com">OnlinePharmacy</a>Friday, 26 October 2007 at 08:50:00 BST

  WEhXXV Your blog is great. Articles is interesting!

  ReplyDelete
 20. <a href="http://m1.aol.com/MacBoyd45/index4.html">jokes about viagra</a>Friday, 26 October 2007 at 19:01:00 BST

  7jXnUg Nice Article.

  ReplyDelete
 21. <a href="http://m1.aol.com/IvySalas33/85_261007.html">meridia mexican pharmacy</a>Friday, 26 October 2007 at 20:14:00 BST

  Please write anything else!

  ReplyDelete
 22. <a href="http://members.ospa.us/portal_memberdata/portraits/thnajtnsq">chicago downtown motel</a>Friday, 26 October 2007 at 20:34:00 BST

  Nice Article.

  ReplyDelete
 23. <a href="http://markas.t35.com/index1.html">casino tour li to ac</a>Saturday, 27 October 2007 at 21:02:00 BST

  Magnific!

  ReplyDelete
 24. <a href="http://unatarka.110mb.com/index9.html">arlo guthrie legacy tour</a>Sunday, 28 October 2007 at 14:38:00 GMT

  Thanks to author.

  ReplyDelete
 25. <a href="http://www.optimising.biz/portal_memberdata/portraits/tldxbgrrg">car loan interest table</a>Tuesday, 30 October 2007 at 06:11:00 GMT

  Good job!

  ReplyDelete
 26. <a href="http://learning.hsc.hccs.edu/portal_memberdata/portraits/tnglpmobm">ringtones</a>Tuesday, 30 October 2007 at 09:25:00 GMT

  Hello all!

  ReplyDelete
 27. <a href="http://www.bcrobotics.org/portal_memberdata/portraits/tunaqpwhm"></a>Tuesday, 30 October 2007 at 13:18:00 GMT

  Thanks to author.

  ReplyDelete
 28. <a href="http://m1.aol.com/EloyRowe59/55-291007.html">order generic cialis</a>Wednesday, 31 October 2007 at 18:28:00 GMT

  AQEUZ1 Please write anything else!

  ReplyDelete
 29. <a href="http://freeringtones.99k.org/free-ringtones-for-lg-verizon-.html">free ringtones for lg ver</a>Wednesday, 31 October 2007 at 18:56:00 GMT

  Hello all!

  ReplyDelete